Makabidhiano ya ofisi TBC kati ya Mkurugenzi Mkuu anayeingia Dk Ryoba na anayetoka Mshana


Mkurugenzi mstaafu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika hilo Dk. Ayoub Ryoba, Taarifa ya Makabidhiano ya ofisi juzi jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi mstaafu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana akizungumza jambo wakati wa sherehe za kuwaaga wafanyakazi wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) na kumkaribisha mkurugenzi mkuu mpya Dkt. Ayoub Ryoba (wa pili kulia) juzi jijini Dar es Salaam. Wengine Pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya TBC Balozi Herbert E. Mrango na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi Bi. Elimbora Muro (wa kwanza kushoto).

Wafanyakazi wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) wakimskiliza Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika hilo Dk. Ayoub Ryoba (hayupo Pichani) wakati alipokuwa akiongea nao juzi jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Dk. Ayoub Ryoba akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo (hawapo pichani) wakati wa kumuaga Mkurugenzi mstaafu wa shirika hilo Bw. Clement Mshana.

Mkurugenzi mstaafu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana (kulia) akimkaribisha rasmi katika ofisi za shirika hilo na kumkabidhi rasmi ofisi Mkurugenzi Mkuu mpya wa shirika hilo Dk. Ayoub Ryoba juzi jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Dk. Ayoub Ryoba akitia saini kitabu cha wageni baada ya kukaribishwa na kukabidhiwa rasmi ofisi za shirika hilo juzi jijini Dar es Salaam.