Mansour Yusuf Himid anashikiliwa na polisi Zanzibar

IDADI ya viongozi wa chama cha wananchi (CUF) kuhojiwa na kushikiliwa na Jeshi la Polisi imeongezeka baada ya Mansoor Yussuf Himid -- aliyekuwa mshauri mgombea chama katika uchaguzi uliopita katika mambo ya siasa wa chama hicho -- kukamatwa kwa mahojiano kuhusiana na kulipuliwa kwa maskani ya CCM, Kisonge, Michenzani mjini Unguja. 

Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui alisema kuwa kiongozi wao Mansoor Yussuf Himid alipokea wito mchana wa jana uliomtaka aende kituo cha Polisi Madema kwa ajili ya mahojiano na kudai kwamba ameshangwazwa kuwa kawekwa ndani.

Kufuatia kadhia hiyo, Mazrui ameliomba jeshi la polisi kutofanya upendeleo na kuegemea upande mmoja katika kutekeleza majukumu yake ya kulinda raia na mali zao.

“Haya ni maonevu makubwa kwani kila uchao tunakamatwa sisi tu bila kujua kosa letu, lakini sishangai sana ndiyo utawala wa kibabe huu,” alisema Mazurui.

Alisema matukio haya yamekuwa yakiendelea kwani juzi ofisi zachama zilioko Mpendae zilivamiwa na kuchukuliwa wananchama wao 30 bila kujua wale wamo katika maeneo yao.

“Wametuvamia katika ofisi halafu wakaharibu kwa kuzichana nyaraka zetu muhimu sana, mhh hatujui hawa wana wanalengo gani kwa kweli,” alillalama Mazurui

Alisema kuwa mara baada ya kutokea tukio hilo, CUF tayari imeanza kuchukua hatua mbadala ikiwemo kuripoti katika jeshi hilo ili kuweza kujua tuhuma zinazowakabili wanachama hao.

Alisema kuwa katika tukio hilo baadhi ya vifaa vilivyokuwemo katika ofisi hiyo ikiwemo computer na mashine ya kutolea chapa (photocopy) viliharibiwa vibaya pamoja na upotevu wa fedha.
  • via blogu ya F. Dande - Habari Mseto