Loading...
Friday

Mchongo wa kuchota fedha BoT ulivyozimwa na Rais

Rais Magufuli na Gavana Ndulu katika ofisi za BoT jana Machi 10, 2016
Rais Magufuli na Gavana Ndulu katika ofisi za BoT jana Machi 10, 2016

Gazeti la MTANZANIA linadai kuwa habari za uhakika ilizozipata jana jioni kutoka kwenye chanzo chake, zinasema fedha kiasi cha shilingi bilioni 925 alizoagiza Rais John Magufuli jana katika ziara yake ya ghafla katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), zilikuwa zimeelekezwa kulipa madeni mbalimbali ya taasisi za Serikali na binafsi.

“Malipo mengi yapo kwenye taasisi ambazo zinatoa huduma serikalini na cheki zao zimerundikana pale wizarani, jambo la kujiuliza kwanini wizara iidhinishe malipo wakati hayako kwenye bajeti.

“Hivi tujiulize wote kama tunaipenda nchi yetu, hivi kweli kwa mtindo huu mwananchi wa kawaida atapata huduma za kijamii,” kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho kilisema BoT na wizara wametakiwa kufuata waraka uliotolewa mwaka 2004 unaotoa mwongozo wa malipo.
 
Toggle Footer
TOP