Loading...
Tuesday

Mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi Uganda - Tanzania

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio akionesha katika ramani njia inayotarajiwa kujengwa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.
MKURUGENZI Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam amesema mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga utaanza mara baada ya hatua mbalimbali za mazungumzo kukamilika.

Alisema ujenzi wa bomba hilo utagharimu dola za Marekani bilioni 4 na bomba litakuwa na urefu wa Km. 1,403 huku uwekezaji huo ukitarajiwa kutoa fursa za ajira zaidi ya watu 10,000 wakati wa ujenzi na watu wapatao 1,000 hadi 5,000 wakati wa kuendesha mradi.

Alizitaja faida za mradi huo ni pamoja na fursa mbalimbali zikiwemo kuongeza wigo wa uwekezaji kwa TPDC na ajira kwa Watanzania pamoja na ushiriki wa kampuni za Kitanzania katika mradi huo.

0 comments :

Post a Comment

 
Toggle Footer
TOP