Loading...
Monday

Polisi yakamata majambazi 5 waliovamia duka la kubadili fedha Masaki, 3 wauawa


JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watu watano ambapo watatu kati ya hao wameuawa katika majibizano ya risasi na polisi.

Akithibiska kutokea kwa tukio hilo leo Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Siro amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa tatu eneo Masaki Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kamishna Siro amesema kuwa watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi waliuawa wakati wakijiandaa kufanya tukio la uhalifu katika moja ya ofisi ya kubadilisha fedha za kigeni iliyopo Masaki.

Amesema kuwa watu hao walikuwa katika gari lenye namba za usajili T 135 AQJ aina ya Toyota, Rav 4 rangi ya kijivu (silver), polisi walilisimamisha gari hilo ndipo majambazi hao wakaanza kurusha risasi na kisha kuzidiwa na kuuawa na polisi waliokuwa katika doria.

Amesema baada ya kuwaua majambazi hao walikwenda kukagua na kukuta bunduki mbili aina ya pisto, hirizi, bomu lakurushwa kwa mkono pamoja na karatasi ambayo ilikuwa imeandikwa maneno katika lugha ya Kiaraabu. 

Siro amesema ametangaza kiama kwa watu wanaotumia nguvu katika utafutaji fedha na kuonya kuwa hawana nafasi tena katika jiji la Dar es Salaam.


 
Toggle Footer
TOP