RC Makonda aendelea kugonga milango kuomba baraka za viongozi wa dini na busara za wazee


Mufti Zubery, akifanya mazungumzo na Makonda.


Dua ikiendelea nyumbani kwa mufti Mikocheni.


Wapiga picha kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

Makonda akiagana na Sheikh Abubakar Khalid na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.

MUFTI wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubery amemuombea dua, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Rais Dk. John Magufuli ili waweze kulitumikia vema taifa na kuliletea maendeleo.

Zubery alimfanyia dua hiyo Makonda Dar es Salaam leo asubuhi alipofika nyumbani kwake kujitambulisha na kumjulia hali pamoja na kumueleza mambo kadhaa ya maendeleo yaliyofanyika.

"Tunakuomba mola wetu kuwapa moyo wa imani na uzalendo na kuwaepusha na mabaya yote Mkuu wetu wa Mkoa Paul Makonda, Rais wetu Magufuli pamoja na viongozi wote ili waliongoze taifa letu kwa amani" alisema Mufti Zubery" wakati akiomba dua hiyo.

Makonda akizungumza na Mufti Zubery nyumbani kwake Mikocheni alimwambia kuwa kuna mambo kadhaa ameyafanya kwa kushirikiana na watendaji wenzake kwa kukutana na waendesha boda boda ili kuwawezesha kupata mkopo utakaowasaidia kupata vitendelea kazi zao kama kupata kofia ngumu mbili za kuvaa dereva na abiria wake ili kuwasaidia katika shughuli zao za kusafirisha abiria.

Makonda alitaja mambo mengine kuwa ni suala nzima la kupambana na uhalifu ambao bado unaonesha kupamba moto hasa ujambazi wa kutumia silaha za moto.

Alitaja mambo mengine kuwa ni mkutano alioufanya hivi karibuni wa kukutana na wenyeviti wa mitaa na maofisa watendaji ili kuzungumzia suala la utunzaji wa mazingira na mambo mengine ambapo alisema ameandaa mpango wa kumzawadia mwenyekiti atakayefanya vizuri kwenye mtaa wake.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum alisema jambo alilofanya Makonda la kumtembea Mufti ni jambo zuri na kuwa kumuona mufti ni sawa kama amewaona waislam wote nchini.

Alisema wanamuombea Makonda mungu amzidishie wepesi katika kazi zake kwani ni viongozi wachache wanaopata madaraka ambao uwakumbuka viongozi wa dini kama alivyofanya Makonda.

Katika hatua nyingine Makonda alifanya ukaguzi wa barabara kadhaa za Manispaa ya Kinondoni ambazo hivi karibuni aliagiza zifanyiwe marekebisho ikiwa ni pamoja na kuchimba mifereji baada ya kuharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.


Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubery akiwa nyumbani kwake.


Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubery (wa pili kushoto), akimuombea dua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum, Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Khalid na Msaidizi wa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Othman Mkambaku.


Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum (kulia), akizungumza na wanahabari kabla ya kufanyika dua hiyo. Kushoto ni Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Khalid.
  • Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com-simu namba 0712-727062


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameanza ziara ya kuwatembelea wazee na viongozi wa dini ili kupata busara zao ambapo jana alimtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kwa ajili ya kupata baraka na busara zake

Siku chache baada ya kuapishwa, Machi 19, mwaka huu alikutana na wenyeviti na watendaji wa mitaa 559 wa Jiji la Dar es Salaam.

Mkuu huyo wa mkoa alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa viongozi hao ili afanye nao kazi kwa ushirikiano na kuja na mikakati tisa, ikiwamo kutenga maeneo ya biashara kwa lengo la kuifanya Dar es Salaam kuwa ya kisasa.

Akizungumza jana, alisema lengo la ziara hiyo ni kujifunza na kuchukua busara kutoka kwa wazee ili zimsaidie katika utendaji wake.

“Mkoa huu una wazee. Ili uweze kuongoza vyema ni lazima upate busara zao zikusaidie katika majukumu yako,” alisema Makonda ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa, leo anatarajia kukutana na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.


Kadinali Pengo akiwa kwenye mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ofisini kwake makao makuu ya Kanisa Katoliki, Forodhani jijini janaKiongozi wa Kanisa la Living Water Centre Kawe Apostle Onesmo Ndegi siku ya jana (Jumapili, Machi 20, 2016) katika ibada amemkabidhi Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda biblia ya Neno la Mungu kwa makusudi ya kusoma Neno hilo kila siku ili liweze kuwa msaada wake katika shughuli za kila siku za Kiserikali!

Ni siku chache tangu Mh. Rais Magufuri ateue wakuu wa Mikoa nchini,hivyo kwasasa majukumu na upinzani kwake utakuwa mkubwa zaidi na mwanzo,hivyo anamhitaji Mungu sana Alisema Apostle Ndegi.Apostle Ndegi aliongeza kwa kusema Mh. Makonda anahitaji maombi ya kila Mtu kwa Mungu ili afanikishe majukumu yake sawasawa.

Mh.Makonda akiongea alisema kila mtanzania kwa nafasi yake lazima ahakikishe anatimiza majukumu yake vizuri tena kwa kufanya kazi ili kuhakikisha maendeleo kwa nafasi ya mtu mmoja na kuacha kutegemea na kusubiri serikali.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Makonda aliongozana na Mke na Mrisho Mpoto katika Ibada hiyo.


Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre Kawe Apostle Onesmo Ndegi

Mrisho Mpoto aliongozana na Mhe.Paul Makonda

Apostle Ndegi akieleza jambo kuhusu Mhe Makonda
Mrisho Mpoto aliongozana na Mhe. Paul MakondaApostle Ndegi akimpa maelekezo kuhusu kusoma Neno la Mungu kila siku maana ndio litamsaidia katika shughuli za kila siku

RC Paul Makonda akiwa na mke wake wakikabidhiwa Biblia ya Neno la Mungu

RC Paul Makonda alipata kuongoza nyimbo ya sifa katika ibada hiyo

RC Paul Makonda alipata kuongoza nyimbo ya sifa katika ibada hiyo

Apostle Ndegi na wachungaji wengine katika Kanisa hilo wakifanya maombi kwa Mh. Paul Makonda

Picha ya pamoja Apostle wa kwanza kushoto, Mhe Makonda, Mke wa Apostle Ndegi ni mke wa Mhe. Makonda