Loading...
Thursday

Siku ya Wanawake: Malaika mlemavu na yatima apata msaada wa kusomeshwa na afya

Mtoto Siwema Ngunga akiwa amekaa kwenye baiskeli yake

Mtoto yatima ambaye pia ni mlemavu (miguu iliyopooza) aitwaye Siwema Ngunga mwenye umri wa miaka minane mkazi wa mtaa wa Madizini mjini Songea mkoani Ruvuma, amepata msaada wa kulipiwa ada ya shule kwa Mwaka Mmoja ambayo ni Shilingi laki tatu na nusu (350,000) kutoka kwa mfanyabiashara wa mjini Songea mkoani Ruvuma, Bi Farida Mdaula pamoja na msaada wa kupata matibabu bure kutoka bima ya afya (NHIF) kwa muda wa mwaka mmoja.


Mfanya Biashara Farida Mdaula akimkabidhi mtoto Siwema Ngunga pesa zilizochangwa na baadhi ya Wanawake waliojitokeza kwenye kilele cha siku ya Wanawake Duniani ambayo ililatibiwa na MM INTERTAIMENT katika ukumbi wa SWISS HOTEL iliyopo Songea Mjini.


Mfanyabiashara Bi Farida Mdaula akitokwa na machozi baada ya kupata historia ya mtoto Siwema Ngunga .


Meneja wa Bima ya Afya NHIF Abdiel E. Mkaro akimkabidhi fomu Siwema Ngunga kwa ajili ya kupatiwa matibabu bure kwa muda wa mwaka mmoja.


Mkurugenzi wa Kampuni ya MM INTERTAINMENT inayoshugulika na watoto waishio katika Mazingira magumu Marietha Msembele ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha habari cha CHANNEL TEN akitowa maelezo juu ya mtoto Siwema Ngunga katika siku ya kilele cha siku ya wanawake duniani


  • Picha na Mpenda Mvula.
 
Toggle Footer
TOP