Taarifa ya Wizara ya hatua iliyofikiwa katika kutekeleza agizo la kuwatoa watumishi hewa

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS


Mtakumbuka kwamba leo ni siku ya 15 ya utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa la kuwataka kuwaondoa kwenye malipo watumishi hewa.

Natumia fursa hii kutoa taarifa kwa Umma kuwa Agizo hilo limetekelezwa kama Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alivyoagiza.

Taarifa za watumishi hewa tayari zimewasilishwa kwa maandishi Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuanzia mwishoni mwa wiki.

Kwa sasa taarifa hizo zinafanyiwa kazi na zitakapokuwa tayari kwa matumizi ya Umma zitatolewa kwa Vyombo vya Habari kwa lengo la kuufahamisha Umma.

Hivi sasa taarifa hizi zinakusanywa kwa pamoja ili kupata idadi kamili.

Wakati huo huo, napenda kuufahamisha Umma kuwa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) yameanza kufanya mazoezi ya utoaji huduma toka siku ya alhamisi tarehe 24/03/2016. Tunategemea wiki hii mtoa huduma ataendelea kuongeza idadi ya mabasi ya kufanya mazoezi kabla zoezi hili halijaanza rasmi.

Imetolewa:
George B. Simbachawene (Mb)
Waziri wa Nchi
29/03/2016.