Loading...
Saturday

Tahadhari kutoka TMA: Mwelekeo wa hali ya mvua Machi - Mei

Dkt. Kijazi (katikati) akitoa taarifa ya mwelekeo wa hali ya mvua nchini. Kushoto ni Samwel Mbuya, Meneja Kitengo Kikuu cha Habari TMA na kulia ni Dkt. Hamza Kabelwa, Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA
Mamla ka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa hadhari kwa wananchi na taasisi mbalimbali ikiwemo za uokoaji, kujiandaa kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za masika ambazo tayari zimeanza kunyesha hapa nchini.

Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Dkt. Agnes Kijazi alitoa rai hiyo juzi Jijini Mwanza, wakati akitoa taarifa ya mwelekeo wa mvua za msimu wa masika kwa kipindi cha kuanzia mwezi Machi hadi Mei, mwaka huu.

Dkt.Kijazi alisema kuwa mvua za masika zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Machi mwaka huu, katika maeneo ya ukanda wa Ziwa na kusambaa katika maeneo mengine yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

Alisema mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi nchini, na kwamba zinaweza kusababisha athari mbalimbali ikiwemo mafuriko hivyo ni vema wananchi pamoja na mamlaka za uokozi zikajiandaa kikamilifu ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.


Mkutano baina ya Wanahabari pamoja na TMA uliofanyika Jijini Mwanza, ambapo TMA ilikuwa ikitoa taarifa ya mwelekeo wa hali ya mvua nchini kwa kipindi cha mwezi Machi hadi mwezi Mei, 2016.


Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
  • Bonyeza hapa kutazama picha za semina kwaa wanahabari.
  • Imeandaliwa na George Binagi - GB Pazzo @BMG

0 comments :

Post a Comment

 
Toggle Footer
TOP