Tanzania na India zasaini mkataba kuwaruhusu wenza wa watumishi Ubalozini kufanya kazi


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Aziz Mlima akizungumza na Balozi wa India nchini Mhe. Sandeep Arya mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara kwa lengo la kusaini Mkataba wa Makubaliano utakaowawezesha wenza wa watumishi katika Balozi za nchi hizi mbili kufanya kazi.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Baraka Luvanda (kushoto) na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Benedict Msuya wakifuatilia mazungumzo na baadae kusimamia zoezi la kusaini mkataba hiyo.

Kushoto ni Afisa kutoka ubalozi wa India ambaye aliambatana na Mhe. Arya

Katibu Mkuu na Mhe. Balozi Arya wakisaini mkataba wa makubaliano baina ya mataifa hayo mawili ambao utaruhusu wenza wa watumishi wa Balozi kutoka Tanzania na India kuruhusiwa kufanya kazi katika nchi hizo.

Wakibadilishana mkataba mara baada ya kukamilisha zoezi la utiaji saini

Wakipongezana baada ya kufanikisha zoezi la kusaini makubaliano hayo.