Loading...
Monday

Wananchi wamkataa Mganga mbele ya Mbunge

Wananchi wa kata ya Ibumu wilaya ya kilolo mkoani Iringa wamemlalamikia mganga wa zahanati ya Ibumu mbele ya mbunge wa Kilolo, Bw Venance Mwamoto kwa madai ya kuwanyanyasa.

Wananchi hao wametoa malalamiko hayo jana wakati wa mkutano wa Mbunge Mwamoto wa  kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao.

Wamesema mganga huyo huyo,   Gasalamwike Mgongolwa hawamtaki katika katakata katika Kata hiyo kutokana na kufanya kazi kwa mazoea na kuwa na visasi kwa wagonjwa.

Pia wametoa malalamiko ya kukosa kupata matokeo ya watoto wao na kero ya pembejeo za ruzuku.

Kwa upande wake, Mbunge Mwamoto amesema kwa suala la mganga huyo atafikisha kwa mwajiri wake ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilolo kwakuwa yeye (Mbunge) hana mamlaka ya kumfukuza.

Akizungumza kwa njia ya simu, Mganga Mgogolwa alidai kuwa tuhuma dhidi yake hazina ukweli kwani anafanya kazi kwa kujituma zaidi, na wapo watu ambao wanaendekeza majungu. Amesema yeye kila siku anafika kazini asubuhi saa 1:30 na kutoka saa 9 alasiri saa kwa mujibu wa taratibu za kazi.
 
Toggle Footer
TOP