Wapigie kura za KORA 2016 Watanzania: Mrisho, Wakazi, Vanessa, Yamoto, Diamond


Tuzo za KORA 2016 zimependekeza wanamuziki wengi wa Tanzania kwa makusudi. Makusudi yenyewe ni kutoa nafasi kwa muziki wa Tanzania kujitambulisha kwa Afrika.

Kwa muda mrefu sasa imeonekana kuwa muziki wa Afrika Mashariki hasa Tanzania kuwa umekosa utambulisho. Kwa mfano ukisikiliza muziki wa Afrika Kusini na Afrika Magharibi ni haraka mtu atajua vionjo vya maeneo hayo. Lakini kwa Tanzania, wengine wanasikika kama Wamarekani, wengine kama Afrika Magharibi nk.

Sasa, muziki wa Tanzania umejipambanua kwa kiasi kikubwa. Na wanamuziki wote walioteuliwa kugombea tuzo za kora wanawakilisha vionjo halisi vya aina mbalimbali kutoka Tanzania. Ni wakati wetu kuonyesha kuwa tunaupenda muziki wetu na tunapedna kuutambulisha Afrika nzima.

Wanamuziki wa Tanzania wakishinda Tuzo za KORA 2016 ni muziki wa Tanzania umeshinda na kujitambulisha katika mataifa mengine duniani.

Mimi nimepiga kura KORA, wewe je; umepiga kura leo? Kura yako moja yaweza kuleta tofauti na heshima ya muziki wa Tanzania. Pigia wanamuziki wetu kura ili muziki wa Tanzania ushinde Tuzo za KORA 2016.

---
Ash K.