Wasemavyo kuhusu Dk Rutengwe aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro


Majadiliano kwenye 'social media' baada ya video iliyopachikwa hapo juu. Mmoja ameandika...
Katika vitu ambavyo siwezi kuvifanya KAMWE ktk maisha yangu ni kujidhalilisha, kujikomba, kujipendekeza au kushusha thamani ya utu wangu kwa sababu tu ya madaraka. Angalia video hii, huyu ni Dr.Rajab Rutengwe (PhD) aliyekua Mkuu wa mkoa wa Morogoro akatemwa kwny uteuzi wa wakuu wa mikoa wapya.

Ameamua kujidhalilisha kwa kiasi kikubwa kwa sababu ya madaraka. Msikilize katika hotuba yake aliyoitoa wakati anakabidhi ofisi kwa Mkuu wa Mkoa mpya Dr.Stephen Kebwe. Dr.Rutengwe anatia huruma, anamuomba Magufuli amhurumie eti anatoka familia duni sana na hana pa kwenda wala pa kushika.

Hivi kweli PhD holder hana pa kwenda? Dr.Rutengwe ana PhD ya Food Security &Technology kutoka Chuo kikuu cha Vaal, South Africa aliyoisomea mwaka 2000 hadi 2004 lakini leo anasema hana pa kwenda. Mbona siasa inatufanya kuuza utu wetu kwa kiasi hiki? Ina maana hadi umri huu alikua hajajiandaa kimaisha hadi aje kulialia kwa Magufuli amhurumie?

Anamnyenyekea Magufuli kama Mungu. Anamuomba Magufuli amhurumie kama vile anaomba sala ya toba.. eti "nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana".. This is bullshit. Unawezaje kumwabudu mwanadamu mwenzio kwa kiwango hiki?

Aisee kanipa hasira sana. Kama wasomi wetu ndio hawa wa kujidhalilisha hivi kuna haja gani ya kusoma sana? Mpuuzi kabisa huyu. Natamani ningekuwepo ukumbini nimkate makofi ya kutosha. Hivi watoto wake, ndugu na marafiki wakimuona anavyojidhalilisha hivi watamfikiriaje? #Big_Shame.!
Mwingine ameandika...
Nimefanya kazi na Dkt Rajabu Rutengwe ni mtu mzuri na mchapa kazi mzuri sana, amekuwa mkuu wa Wilaya Ulanga amefanya kazi mzuri sana,akapanda Ukuu wa Mkoa akaenda Katavi nako alifanya kazi mzuri sana kabla hajahamishiwa Tanga ambako hakukaa sana kabla hajaletwa Morogoro mimi nikiwa Dc kilombero.

Kauli alizotoa siku anakabidhi ofisi ni Kauli za kusikilizwa mara mbili na sio kama tafsiri za baadhi ya watu kwamba Dkt hana la kufanya baada ya kutemwa kuwa Mkuu wa Mkoa.

Matatizo ya wakulima na wafugaji ndani ya Mkoa wa Morogoro yameanza muda na yataendelea kama serikali haitochukua hatua za makusudi za kutenga pesa Kwa ajili ya kusimamia mipango bora ya Ardhi,kujenga majosho na kuanzisha ranchi za kisasa ambazo zitaondoa muingiliano kati ya wafugaji na wakulima.

Kama pesa hazitatengwa hata akipelekwa Brigedia wa jeshi watu bado wataendelea kupigana tu kutokana na kutafuta mahitaji Kwa ajili ya mifugo ambayo inaendelea kuongezeka siku hadi siku wakati Ardhi haiongezeki

Wakuu wa mikoa walioachwa ni wengi lakini aliyetolewa sababu za kuachwa ni mmoja tu, hapa ndio pametengeneza maswali mengi sana Kwa Dkt ndio maana ameona aombe radhi kama amekosa Kwa jambo ambalo ni la kimfumo ambalo halikutokana na uzembe wake.

USHAURI

Ili Wakuu wa mikoa wanaopelekwa Morogoro wasionekane wazembe ni lazima serikali ya awamu ya tano ni lazima itenge bajeti maalum na itengeneze kikosi kazi ambacho kitazama ndani kushugulikia masuala ya wafugaji na wakulima

Nakutakia kila la kheri Dkt Rutengwe wewe ni kiongozi na mwenyezi mungu atakuvusha ktk kipindi hiki.

Mwl Masala
Nachingwea