Waziri akabidhiwa na Wakuu wa Mikoa orodha za "malipo kwa watumishi hewa"

Waziri Simbachawene akizungumza na Wakuu wa Mikoa leo jijini Dar es Salaam

MKOA Mwanza unaongoza kuwa na watumishi hewa 334 ukifuatiwa na mkoa wa Arusha (270) kati ya watumishi hewa 2,702 waliobainika kulipwa mishahara katika nchi nzima.

Hata hivyo Shinyanga na Songwe ni mikoa isiyokuwa na watumishi hewa. Kukosekana kwa watumishi hewa katika mkoa wa  Shinyanya imetokana na mikakati ya mikoa hiyo kila idara kupeleka majina ya watu wanaostahili kulipwa mishahara kila mwezi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Killango amesema kuwa viongozi walioanza katika mikoa huo walijipanga katika kuondokana na watumishi hewa.

Mkoa wa Songwe kukosekana kwa watumishi hewa kunatokana na upya wake na mkuu wake mkoa ameapishwa wiki moja iliyopita.

Akizungumza na Wakuu wa Mikoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI, George Simbachawene aliwataka wakuu wa mikoa wafanye kazi ikiwemo ubunifu wa miradi ya kuongeza mapato.

Simbachawene amewataka wakuu wa mikoa kuondokana na matumizi yasiyo ya lazima ili fedha hizo zitumike katika matumizi ya msingi.

Amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu ikiwa ni pamoja na kushughulika na watoro ambao wanalipwa fedha wakati hawafanyi kazi.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri ametaka wote waliohusika na hujuma za mishahara wafikishwe katika vyombo vya dola na tayari mkoa wake umeanza kutekeleza hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza baada ya kukabidhi
HATIMAYE wakuu wa Mikoa yote nchini wametii agizo la Rais John Magufuli lilokuwa linawataka wasilishe ripoti ya idadi ya watumishi hewa kwenye mikoa husika.

Wakuu hao wa mikoa wapya wamewasilisha ripoti za watumishi hao leo Jijini Dar es Salaam,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Georgy Simbachawene ili kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watumishi waliohusika katika kashfa hizo,

Mkoa wa Dar Es Salaam.

Akiwasilisha ripoti ya watumishi hewa.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema katika mkoa wake baada ya kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na kamati mbali mbali wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa 73 ambao watumishi hao hewa wamepelekea serikali kupotea pesa zaidi ya Milioni 316 kwa mwaka mmoja.

“Katika mkoa huu tumepata watumioshi hewa 73, ila wengi watahoji mkoa huu mkubwa kwa nini unakuwa na watumishi hewa wachache, nakata kukwambia Waziri, bado tunaendelea na uchunguzi wa kina,” amesema Makonda .

Mkoa wa Arusha.

Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Felix Ntibenda amesema katika mkoa huo umegundurika kuwepo na watumishi hewa 270 ambao wamekuwa wakiisababishia hasara serikali ya Bilioni 1.8 kwa kipindi cha Mwaka mmoja,

Mkoa wa Dodoma.

Pia Mkuu wa Dodoma Jordan Rugimbana amesema katika mkoa wake wamegundua kwenye mkoa huo kuna watumishi hewa 101 ambao amedai wameisabishia hasara serikali milioni 287.3 kwa kipindi cha miezi sita.

Mkoa wa Iringa.

Mkoa wa Iringa Amina Masenza amesema katika mkoa wake wamegundua kuwa kuna watumishi hewa 15 ambapo amemweleza Waziri Simbachawene kuwa licha hao kuna watumishi 145 ambao hajaonana nao huku akidai kuwa akimaliza kuonana nao huwenda idadi ya watumishi hewa ikaongezeka.

Mkoa wa Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenelal Mstaafu Salum Kijuu amesema mkoa wake wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa 14 ambao wamesababisha upotevu wa pesa za serikali Milioni 49.1

Mkoa wa Katavi.

Pia Mkuu wa mkoa huu, Jeneral Raphael Muhuga amesema mkuo huo umegundurika kuwepo kwa watumishi hewa 21 ambao wameitia hasara serikali Milioni 20.7.

Mkoa wa Kigoma.

Pia Mkoa wa Mkuo huyo, Bregedia Jenaral Mstaafu Emmanuel Maganga amesema katika mkuo huo wamebaini kuwepo watumishi hewa 171 ambao wameitia hasara serikali milioni 114.6.

Mkoa wa Kilimanjaro.

Mkuu wa Mkoa huo,Merck Sadick amesema wamebaini mkuo wake umegundurika kuwepo na watumishi hewa 111 ambao wamekuisababishia hasara serikali hasara ya milini 281.4.

Mkoa wa Lindi

Kwa Upande wa Mkuu wa mkoa huo,Godfrey Zambi amesema mkoa wake unawatumishi hewa 57 ambao wameitia hasara serikali milini 36.2.

Mkoa wa Manyara.

Kwa Upande wake mkuu wa mkoa huo,Joel Bendera, amesema mkuo umekuwa na watumishi hewa 42 ambao wameitia hasara serikali Milioni milioni 313.9.

Mkoa wa Mara.

Kuhusu Mkuoa wa Mara,Mkuu wa mkoa huo,Magesa Mulongo amesema katika mkoa wake wamebaini kuna watumishi hewa 94 ambao wameitia hasara serikali milioni 121.

Mkoa wa Mbeya.

Kwa upande wa Mkoa wa Mbeya,Mkuu wa Mkuo huo,Amos Makalla amesema katika mkoa wake kumekuwa na watumishi hewa 98 ambao pia wameitia hasara serikali Milioni 459 .6.

Mkoa wa Morogoro.

Hata hivyo mkuu wa mkoa huo,Dkt Steven Kebwe,ambapo amesema mkoa wake umegundurika kuwepo na watumishi hewa 122 ambao wameitia hasara serikali milioni 450.7.

Mkoa wa Mtwara.

Mkuu wa mkoa huo, Halima Dendegu amesema mkoa wake ubainikika kuwepo kwa watumishi hewa 17, huku watumishi wengine 285 uchunguzi ukiendelea, ambapo watumishi hao 17 wameitia hasara serikali milioni 216.5.

Mkoa wa Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa John Mongella amesema mkoa wake umengundurika kuwepo kwa watumishi hewa 334.

Mkoa wa Njombe.

Mkuu wa Mkoa wa NJombe,Dkt Rehema Nchimbi amesema mkoa wake umekuwa na watumiwa na hewa 34 ambao amedai wamekuwa wakiitia hasara serikali Milioni 20.1.

Mkoa wa Pwani.

Mkuu wa Mkoa huyo,Mhandisi Evarist Ndikilo amesema Mkoa wake umekuwa na watumishi hewa 150 huku hakishindwa kusema hasara ya fedha za serikali kwa madai kuwa uchunguzi unaendelea.

Mkua wa Rukwa.

Mkuu wa mkoa huo,Kamishna Mstaafu Zerote Steven amesema mkoa wake umekuwa na watumishi hewa, 18 na wametia hasara serikali milioni 55.6.

Mkuo wa Ruvuma,

Mkuu wa Mkoa huo,Thabiti Mwambungu amesema mkoa huo umekuwa na watumishi hewa 35 ambao wameitia hasara serikali milioni 58.4.

Mkoa wa Simiyu.

Mkuu wa Mkoa huo,Antony Mataka amesema mkoa huo umegundurika watumishi hewa 62 wameitia hasara serikali ya Milioni 320.9.

Mkoa wa Singida,

Mkuu wa mkoa wa huo,Mhandisi Methew Mtigumwe amesema kuwa wafanyakazi hewa katika mkoa wake,231 nakueleza kuwa uchunguzi bado unaendelea ili kubaini zaidi.

Mkoa wa Tabora

Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameanisha kuwa katika mkoa wake watumishi hewa 48 ambapo wanaitia hasara Serikali Milioni 118.7.

Mkoa wa Tanga.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela amesema kuwa watumishi hewa katika mkoa wake ni 104 ambapo amesema kuwa tathimini ya kuhakiki bado inaendelea.

Hata hivyo katika mkoa wa Shinyanga imekuwa tofautina mikoa mingine ambapo hadi sasa hakuna watumishi hewa kutokana na mikakati iliyowekwa na kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 na mkuu wa mkoa aliyepita.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadik akikabidhi majina hewa kwa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene baada ya kumkabidhi majina watumishi hewa, jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora , Aggrey Mwanri akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.


Wakuu wa Mikoa na Watendaji wa TAMISEMI wakimsikiliza Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.