Loading...
Tuesday

ACT-Wazalendo yateua wa Kaimu Katibu Mkuu kuchukua nafasi iliyoachwa na Mwigamba


MAAZIMIO YA HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO KUFUATIA KIKAO CHAKE CHA JUMATATU TAREHE 25 APRILI 2016

Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha ACT-Wazalendo ilifanya kikao chake cha kawaida jana (Jumatatu) tarehe 25 Aprili 2016 Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu:
  1. Ilimteua Ndugu Juma Saanani kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Chama hadi pale uchaguzi mkuu wa ndani ya chama utakapofanyika. Uteuzi huu unafuatia kung’atuka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Ndugu Samson Mwigamba anakwenda masomoni katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Juma Saanani alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama (Zanzibar).
  2. Ilipitisha Mpango Mkakati wa Chama utakaongoza programu za chama kwa kipindi cha miaka mitano (2016-2020).
Aidha, kwa kuzingatia mamlaka yake kikatiba (Ibara ya 29 (25iv), Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe (MB) amemteua Ndugu Samson Mwigamba kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Chama na Kamati Kuu imekwisharidhia uteuzi huo. Uteuzi huu umefanyika kwa kuzingatia kuwa Mwenyekiti wa Kamati halazimika kufanya kazi makao makuu na hivyo Ndugu Mwigamba ataendelea na masomo yake bila kikwazo.

Ado Shaibu
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kuwa Umma.
Jumanne, 26 Aprili 2016

0 comments :

Post a Comment

 
Toggle Footer
TOP