Akizungumza na baadhi ya wananchi katika stendi ya mabasi ya zamani wakati wa kuweka mapipa hayo ,mkuu wa wilaya alisema zoezi hilo lilitakiwa lifanyike saa 1.30 asubuhi lakini wamelazimika kufanya saa 3.30 kutokana na uzembe uliofanywa na injinia ambaye alipewa kazi ya kuandaa kokoto na mchanga mapema matokeo yake hakufanya hivyo.
“Kwanza aliagizwa na Mkurugenzi wa manispaa hiyo Lewis Kalinjuna kufanya maandalizi mapema ya vitu vinavyotakiwa kwenye kazi ya kuweka mapipa ya taka nyepesi,matokeo yake mpaka leo asubuhi hakuna kilichofanyika hak una kokoto wala simenti eneo la kufanyika kazi huu ni uzembe , mkuu wa kituo uko wapi kamata huyu muweke ndani”aliagiza mkuu wa wilaya.
Hata hivyo mkuu wa wilaya aliwataka wananchi kuyatumia kwa kuweka taka nyepesi huku akiwatahadharisha wafanyabiashara wa vyuma chakavu, kuwa makini na watu wanaowauzia vyuma hivyo na kuwafichua watakao yaharibu na kwenda kuuza wakibainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Alisema iwapo mazingira yatakuwa katika hali ya usafi jamii haiwezi kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu na magonjwa mengine ,nakusisitiza kuwa suala la usafi linatakiwa kuwaendelevu kuanzia sehemu wanayoishi, kwenye biashara na maeneo yanayowazunguka.
Awali akijitetea mhandisi huyo wa manispaa Ngagani alisema tatizo lililofanya achelewe kufanya maandalizi ni kutokana na kukosa fedha za kununua kokoto na simenti na kulazimika kuanza kuomba kwa wadau na kufanikiwa kupata muda ukiwa umeenda.
Kwa upande wake ofisa afya wa manispaa hiyo Elly Nakuzerwa alisema jumla ya mapipa 50 ya kuweka taka nyepesi yametolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo, ikiwa ni kuhakikisha mji unakuwa katika hali ya usafi na kujiepusha na mlipuko wa magonjwa kikiwemo kipindupindu.
Aliwatahadharisha wananchi kutoweka mabaki ya vyakula kwenye mapipa hayo na kuwataka kuzingatia usafi kwa kila mmoja, ambapo atakayebainika anatupa uchafu hovyo atatozwa faini ya papo kwa papo sh 50,000 na akishindwa anapelekwa mahakamani.
- via Kareny blog