
MAGARI zaidi ya 1500 jana yalikwama kwa zaidi ya saa tisa katika eneo la Chalinze Nyama wilaya ya Chamwino.
Miongoni mwa magari hayo ni mabasi na malori.
Adha hiyo imegusa magari yote yanayotoka mikoa ya Kanda ya Ziwa Mwanza na mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa HabariLeo, Sifa Lubasi kulikuwa na msongamano mkubwa wa magari zaidi ya kilomita 10 kutoka upande
moja kwenda upande mwingine.
Mafuriko hayo yalisababishwa na mvua iliyonyesha kuanzia jana jioni na kusababisha barabara kujaa maji kiasi cha njia kushindwa kuonekana.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana ambaye alifika eneo la Chalinze Nyama kujionea hali halisi aliwasihi madereva kuchukua hatadhari ya hali ya juu pindi wanapopita kwenye eneo lililojaa maji.
Mafuriko hayo kutoka maeneo ya milimani kata ya Hombolo yalianza kujaa barabarani na maeneo ya kuzunguka nyumba za wakazi wa kijiji cha Chalinze Nyama, yaliwafanya wenyeji kukaa nje maeneo
ya mwinuko wakiwamo akina mama na watoto wao wadogo pamoja na wazee.
Takribani kaya zisizopungua mia moja zimeathiriwa na mafuriko hayo.
Barabara hiyo kuu ilifungwa kwa muda kuanzia saa 12:00 alfajiri hadi alasiri baada ya maji kupungua ndipo yaliporuhusiwa kuendelea na safari.
“Ilipofika saa nne nne hivi kuna basi lilijaribu kupita lakini likaserereka abiria wakatokea madirishani baada ya hapo hakuna gari ambalo limeruhusiwa kupita mpaka sasa” alisema mkazi mmoja wa Chalinze Nyama.
Aidha familia inayosadikiwa kuwania ya shekhe wa Msikiti wa Jumuiya ya Ahmaddiyya uliopo kijijini hapo jirani na barabara itokayo Dodoma kwenda Dar Es Salaam, walijikuta nyumba yao imezungukwa na maji ya mafuriko hayo nakushindwa kutoka nje hadi jeshi lazima moto kutoka Dodoma Mjini walipokuja kuwanusuru.
Pia mvua hiyo imesababisha miundombinu ya umeme hususani nguzo zinazosambaza umeme kwenye kijiji hicho kwenda hadi wilayani Kongwa kuanguka na kusababisha umeme kukatika.

Majira ya saa 9 alasiri ya jana, magari yalianza kupita katika eneo ambalo lilikuwa limefurika maji na uongozi wa Chamwino kuzuia magari kupita, eneo la Chalinze.
Mkuu wa mkoa Jordan Rugimbana alifika eneo la tukio na kuwafariji waathirika.
Kwa mujibu wa TBC magari hayo yalitanda zaidi ya kilomita mbili kila upande na kuleta msukosuko mkubwa.
Mkuu wa mkoa Jordan Rugimbana alifika eneo la tukio na kuwafariji waathirika.