Loading...
Thursday

Jiji la Dar lampata Naibu Meya

Jiji la Dar es Salaam limempata Naibu Meya, Musa Kafana kutoka chama cha wananchi, CUF, baada ya kupata ushindi wa kura 10 kati ya 16 zilizopigwa.

Kafana akishukuru wapiga kura amesema analifahamu jiji vizuri na yupo tayari kuwaletea wananchi mabadiliko kwa kasi ya Rais John Magufuli.

Mpinzani wake, Mariam Mohammed kutoka CCM alipata kura 6.

Idadi ya wapiga kura iliyotarajiwa ilikuwa ni wajumbe 18.
 
Toggle Footer
TOP