Kijana wa miaka 25 Dar ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kulawiti

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, imemuhukumu, Omary Hamis (25) mkazi Gongo la mboto Dar es Salaam kutumikia kifungo cha maisha jela, baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka tisa ambaye ni bubu na kiziwi (jina linahifadhiwa).

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Flora Haule, kufuatia kukamilika kwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka ambao ulikuwa na mashahidi tisa.

“Mahakama inatoa hukumu kwa mtuhumiwa kwa kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mvulana wa miaka tiza mwenye ulemavu wa kusikia na kuzungumza, ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo,” alisema Hakimu Haule.

Awali katika utetezi wake juu ya kwanini asipewe adhabu kali, Hamisi alidai kuwa, anafamilia inayomtegemea hivyo apunguziwe adhabu maombi ambayo yalitupiliwa mbali na mahakama hiyo.

Wakili wa Serikali, Ester Kywara aliiambia mahakama hiyo kuwa hakukuwa na rekodi za mashtaka ya nyuma dhidi ya Hamis na hivyo kuiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wote wanaotumia mabanda ya kuonyesha Vide kufanya ukatili kwa watoto hasa wenye ulemavu, kuwa sheria ipo na itachukua mkondo wake kwa yeyote atakayebainika.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Agost 26 mwaka 2014 Gongo la mboto jijini Dar es Salaam, Hamis alimlawiti mtoto huyo mwenye miaka tisa ambaye ana ulemavu wa kusikia na kuongea jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mtoto huyo siku ya tukio alifika kwenye banda la kuonyeshea video ambalo linamilikiwa na hamisi saa za jioni kwaajili ya kutaka kuangalia video, lakini Hamis alimtimulia mbali kutokana na mtoto huyo kutokuwa na pesa ya kiingilio.

Baaada ya kumfukuza mtoto huyo aliondoka lakini baadaye alirudi bila, Hamis kuwa na taarifa ambapo alikaa ndani humo na kisha kupitiwa na usingizi uliopelekea abaki peke yake ndani humo hadi usiku.

Kutokana na hali hiyo ya kupitiwa na usingizi mpaka usiku, Hamis alitumia mwanya huo kumlawiti mtoto huyo kwenye jumba bovu lililopo jirani na ofisi yake hiyo.

Shahidi namba moja na namba waliiambia mahakama hiyo kuwa walisikia sauti ya mtu aliyekuwa akiomba msaada ambayo uilikuwa haisikiki, ndipo waliposogea na kumkuta, Hamis akitekeleza unyama huo.

Waliiambia mahakama hiyo kuwa, hata walipomkaribia, Hamis bado aliendelea kutekeleza unyama huo hadi walipolazimika kumpiga teke.

Hamis, alikili ushahidi huo uliowasilishwa mahakamani hapo na kuongeza kuwa ni kweli kuwa siku hiyo watoto walifika kwenye banda lake hilo.

Daktari pia aliithibitisha juu mtoto huyo kufanyiwa unyama huo, sanjari na kidhibiti cha Pf3.