Loading...
Thursday

Mahiga, USA Amb. Childress meeting

Wakati misaada ya Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), ikisitishwa, Marekani imeihakikishia Tanzania bado itaendelea kupata Dola 700 milioni ambazo ni sawa na Sh152 trilioni katika kufadhili miradi ya afya na elimu.

Katika Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje,Afrika Mashariki,Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa Dr Augustine Mahiga na Balozi wa Marekani nchini Mark Childress kilichofanyika juzi, lengo lilikuwa ni Tanzania kutaka kuhakikishiwa iwapo miradi inayofadhiliwa na Marekani nchini kama bado nchi hiyo itaendelea kuifadhili ama itasitishwa.

Hata hivyo, Balozi huyo wa Mareani nchini alimuhakikishia Waziri Mahiga kuwa licha ya changamoto mbali mbali za kisiasa zilizopo nchini, bado nchi yake imeona umuhimu wa kuendeleza mahusiano katika kutoa misaada ya maendeleoa hasa katika sekta ya elimu na afya.

 
Toggle Footer
TOP