Loading...
Saturday

Mawakala 2 mahakamani kwa kusafirisha kemikali zenye vionvyo vya dawa za kulevya

MAWAKALA wa Usafirishaji, Revocatus Musuli (45) na Timothy Nilila (43), wakazi wa Tabata Kinyerezi, jijini Dar es Salaam, wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa kujibu shitaka la kusafirisha kemikali zenye vionjo vya dawa ya kulevya kwenda Pakistan.

Washtakiwa hao walisomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa.

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa kati ya Oktoba 5 na 23, mwaka jana, katika Bandari ya Dar es Salaam wilayani Ilala, washtakiwa walikutwa wakisafirisha kemikali aina ya Acwtic Anhydride na Acetic Comprising.

Ilidaiwa kuwa kemikali hizo zilifungwa kwenye mamboksi 880 yenye uzito wa kilo 22,000 zikiwa na vionjo na madhara kama dawa za kulevya wakifarisha kwenda Pakistan.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa kesi hiyo upelelezi utakapokamilika itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusikilizwa.

Hakimu Riwa alisema kesi hiyo itatajwa Aprili 14, mwaka huu na aliamuru washtakiwa wapelekwe mahabusu.
 
Toggle Footer
TOP