Loading...
Monday

Msisimko wa Watanzania na daraja lao la Kigamboni


Daraja la ksiasa la Kigamboni linalounganisha eneo la Kigamboni na upande wa Kurasini likikatisha bahari ya Hindi. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kulizindua rasmi daraja hilo Jumanne Aprili 19, 2016.

Daraja la Kigamboni lililopo jijini Dar es Salaam, ndilo daraja refu zaidi Afrika Mashariki linalobeba uzito kwa nyaya au kamba kuvuka bahari.


video: BBC SwahiliNa K-VIS MEDIA/Khalfan Said, Kurasini

ZAMANI kwa mgeni aingiae jiji la Dar es Salaam, ataambiwa “Kashangae Ferry” lakini mgeni atakayeingia leo jijini, ataambiwa "Kashangae Kurasini - daraja la Kigamboni".

Hiyo ndiyo hali halisi ilivyokwa sasa ambapo mamia yawakazi wa jiji wamekuwa wakienda kwenye Daraja la kisasa la Kigamboni mosi kushangaa maajabu ya daraja lenyewe ambalo ni refu kuliko madaraja yote hapa nchini pengine Afrika Mashariki, lakini pili kupiga picha za kisasa “selfie”.

Daraja hilo lenye urefu wa mita 680 likiunganisha eneo la Kigamboni na Kurasini wilayani temeke jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa za wakandarasi wa mradi huo, Daraja hilo litakuwa na barabara sita, tatu kila upande, na pia njia za waenda kwa miguu (pedestrians).

Hali pametengwa milango kwa ajili ya matumizi ya magari aina tofauti.

Geti namba 1 ni kwa wale wenye vibali maalum, geti namba 2, geti namba 3 na geti namba 4 ni wenye magari madogo binafsi, geti namba 5 ni minibus (daladala) na geti namba 6 ni maalum kwa malori.

Daraja hilo ambalo ujenzi wake umeanza Februari 1, 2012 ni mradi wa ubia kati ya Serikali yenye asilimia 40 na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, NSSF yenye asilimia 60.

Daraja hilolinaongeza vivutio vikuu viwili ambavyo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam inavyo, daraja lenyewe la Kigamboni lakini pia uwanja wa kisasa wa taifa.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kulizindua rasmi daraja hilo Jumanne, Aprili 19, 2016 na tayari maandalizi ya hafla hiyo yanaendelea ambapo K-VIAS MEDIA, imezuru eneo hilo leo Aprili 18, 2016 na kujionea wajkandarasi na maafisa wa serikali wakiweka mambo sawa tayari kwa shughuli hiyo muhimu katika historia ya nchi hii.

Lakini pia ukitaka kuona mfano wa “flyover” basi pitia hapo Kurasini uone jinsi barabara zilivyobebana kuelekea eneo la daraja na zile zinazoungana na barabara ya Mandela.
Akinamama hawa na watoto wao walikuwa ni miongoni mwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanaofika "kulishangaa" daraja hilo la kisasa

Barabara inayoelekea kwenye daraja hilo
  • Picha zote: K-VIS MEDIA/Khalfan Said
Zifuatazo ni kutoka vyanzo vingine vya habari...
0 comments :

Post a Comment

 
Toggle Footer
TOP