Loading...
Saturday

Mwalimu Mndeme: Milioni 50 kwa kila Kijiji - Sehemu ya Pili

Mtaji wa milioni 50 kwa kila kijiji utumike kujenga Tanzania yenye Viwanda: Sehemu ya Pili


Ni wazi kwamba serikali haiwezi kuwekeza kwenye viwanda bila ushirikiano na jitihada za makundi mbalimbali ya wadau wa maendeleo kuanzia na mtu mmoja-mmoja, makundi ya kijamii, wafanyabiashara, wanazuoni, na sekta binafsi kwa ujumla wake. Kila mwenye uzalendo na mapenzi mema na nchi yetu analazimika kusaidia utekelezaji mzuri wa sera na mipango ya serikali maana mafanikio yake ni yetu sote na anguko au hasara yake ni yetu sote. Ni lazima kuishauri, kuikosoa, na kuiwezesha serikali ili iwe na mikakati mizuri inayotekelezeka katika kutimiza matamanio yetu ya kuimarisha uchumi wa viwanda. Pili ni lazima serikali ione umuhim wa jinsi ambavyo twaweza kutumia rasilimali na mitaji tuliyonayo kwa umakini na kimkakati ili kufanikisha ndoto ya viwanda.

http://i1.wp.com/dar24.com/wp-content/uploads/2016/01/Noti-Bandia.jpg?resize=745%2C447

Makala hii ni mwendelezo wa sehemu ya kwanza ambayo niliahidi kutoa mapendekezo ya namna ya kutumia mtaji wa uwezeshaji kiuchumi wananchi wa kugawa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji ili utumike katika kuwezesha utekelezaji wa mkakati wa kujenga Tanzania yenye uchumi wa viwanda. Kwa kuwa nia ya kuanzisha au kuimarisha viwanda tunayo, na Rais hajabadilisha msimamo wake tangu alipoanza kampeni za kuelekea  Magogoni kuhusu “Tanzania ya Magufuli yenye uchumi wa viwanda”, tuna hakika kwamba jambo hili lina msukumo, morali, ushawishi, uongozi thabiti, na mahali pa kuanzia tofauti na serikali iliyopita. Hata hivyo kunahitajika fikra, tafakuri, ubunifu na mikakati thabiti ili kuifanya ndoto hii kuwa halisia. Kwa kuanzia, tuna milioni 50 tunazotegemea kuzigawa kwa kila kijiji.

Jana nimemsikia Naibu Waziri anayehusika na Kazi (Mh Mavunde) akielezea bungeni kwamba fedha hizi zilizoahidiwa kwa kila kijiji, zinategemea kugawanywa mwaka ujao wa kazi na serikali kupitia wataalamu wake, inatazama namna bora za ugawaji na fedha hizi. Kwa kuwa mpango huo ndio unaandaliwa, huu ni wakati muafaka wa kuishauri serikali ili wataalamu hawa wasifanye maamuzi na kutoa ushauri ulifungiwa ndani ya “boksi la mikopo na ujasiriamali” pekee, na badala yake wajue ziko njia nyingine zinazoweka kutumika kwa tija kubwa na yenye hakika zaidi. Inawezekana namna bora inayofikiriwa ikaishia kuwa jinsi ya kuzigawa kupitia vyama vya ushirika, vyama vya kuweka na kukopa, makundi ya uzalishaji mali, na biadhara ndogondogo. Mimi napendekeza nini?


Mimi nanapendekeza kwamba mtaji huu wa Shilingi Milioni 50 kwa kila kijiji tumike katika “Uanzishaji wa Viwanda vya vidogo vya usindikaji mazao (malighafi) zipatikanazo eneo husika (Establishment of small and localized processing-industries)”

http://cdn0.myopensign.com/assets/pact/brickwood-v2-site/w1YPTl4dczTrVax/web.Infini-transparent-background-2lt-3lt.png
http://typostrate.com/wp-content/uploads/2013/09/tumblr_msz3qhHhls1qgnue7o8_1280.jpg
http://www.rondo-ganahl.com/website/uploads/images/10/660x/apfelkiste_08.jpg?v=2
http://zg-brand.ru/images/Top_-10/jam/2-jam-packaging-design.jpg
http://www.sunnforest.com/Packaging/images/Mesh-Nets.png
http://www.packworld.com/sites/default/files/styles/lightbox/public/field/image/CaseReady.jpg?itok=rP2TkyAN


Hili lifanyikaje?
 1. Badala ya kugawa fedha hizi wahitaji ni wengi vijijini kama mtaji mdogomdogo, tuzigawe kwa wilaya au majimbo ya uchaguzi. Kwa kufanya hivyo tutakua na hakika kwamba kila wilaya ina mtaji wa fedha zisizopungua billion 6.5 kama mtaji wa uwekezaji (rejea makala sehemu ya kwanza)
 2. Hata kabla ya kupatikana fedha hizi, serikali iunde timu ndogo ya wataalamu wasomi na wajuzi wa uwekezaji wasiozidi kumi na kundi hili lijigawe kupata timu mbili. Timu hizi zitembelee wilaya zote Tanzania na kurejea taarifa zilizoko, historia ya uzalishaji na rasilimali zinazopatikana nchini, na maandiko/machapisho mbalimbali yanayoelezea rasilimali na uzalishaji mali kwa kila wilaya. Kazi hii ifanyike mapema iwezekanavyo na isizidi miezi miwili kwani kwa sehemu kubwa taarifa zipo inagwa haziapangaliwa vizuri.
 3. Baada ya kupata taarifa sahihi zitokanazo na namba (2) hapo juu, timu hizi zipendekeze kwa serikali ni aina gani ya uzalishaji wa viwanda vidogo-vidogo na vya kati unaweza kufanyika kwa kila  wilaya kulingana na rasilimali/malighafi zilizoko katika eneo husika.
 4. Kutikana na namba (3), timu hii itategemewa kuja na mapendezo yenye uhalisia na yasiyo ya kufikirika. Kwa mfano:
  1. Kwa wilaya zinazolima mazao ya nafaka, mandekezo yajikite katika  uanzishwaji wa viwanda vya kukoboa, kusindika, kufungasha, na kuhifadhi vyakula kama unga, mchele, ngano, nk.
  2. Kwa wilaya zinazofuga mifugo kama ngombe kwa wingi, mapendekezo yawe  viwanda vya kuchinja, kufungasha, kuongeza thamani, na kuhifadhi nyama, kutengeneza ngozi, kufuga ng’ombe bora wa maziwa na kupaki maziwa masafi kitaalamu kwenye vyombo vya ujazo tofautitofauti, kutengeneza siagi, nk.
  3. Kwa wilaya zenye kuku wengi kama mikoa ya kati, tuone viwanda vya kuhifadhi na kupaki mayai, kuchinja na kupaki kuku, mayai, nk.  
  4. Wilaya zenye matunda ziwe na viwanda vya kutengeza juice mbalimbali, vyakula vya matunda, vyakula vya mifugo, nk.
  5. Wilaya ambayo ni miji inaweza kuwekeza katika usindikaji wa taka ngumu na kutengeneza vitu kama mbolea, nishati, na recycling za bidhaa kama za plastic na vyuma.
  6. Penye maji mengi, kuznishwe skimu za umwagiliaji kuzalisha vyakula mbalimbali
  7. Kwenye miti wawe na bidhaa za mbao, toothpicks, furniture za kisasa na bidhaa zinginezo. Tufanye hivyo kwa uvuaji samaki, kwenye madini, nk.
 5. Kutokana na mapendekezo ya namba (3 na 4), iundwe timu ndogo ya wataalamu na wanazuoni kufanya utafiti na kupata makadirio ya gharama za uwekezaji inayohitajika kwa ajili ya uanzishwaji wa viwanda husika (mitambo na miundombinu ya lazima). Nasisitiza kwamba viwanda hivi viwe vidogo kulingana na mtaji ulioko.
 6. Baada ya kupata makisio ya gharama za mwanzoni, Wataalamu hawahawa, wapewe wajibu wa  kushikiana na kila wilaya husika kupitia halmashauri zao kuanzisha viwanda husika huku wakishirikisha wananachi. Iwapo tutaona tutahitaji kiwanda kikubwa au kuwa na tija zaidi iwapo uwekezaji utakua wa fedha nyingi kidogo kuliko zinazopatikana, twaweza kuwa na kiwanda kimoja kinachotumia rasilimali zinazopatikana kwenye wilaya mbili au tatu zinazopakana na zinazozalisha mazao yanayofanana. Ikiwa ngumu kabisa, hata wilaya za mkoa mmoja zote zitumie mtaji wao kwa kiwanda kimoja iwapo ni lazima kufanya hivyo kwa uzalishaji wenye tija
 7. VETA na vyuo vingine vya ufundi kama vinavyotoa FTC, vitakiwe kuzalisha mafundi mchundo (wataalamu) watakaofanya kazi kwenye viwanda hivi. Pili wasaidie kutengeneza mitambo, mashine  na spea zitakazoitajika kwenye viwanda hivi
 8. Msisitizo uwekwe kwa wananchi kuzalisha malighafi zinazohitajika kwenye viwanda hivi kwa matumaini kwamba soko la usindikaji litakua karibu nao na ni la hakika zaidi
http://crossriverwatch.com/wp-content/uploads/2014/04/groundnut-oil-machine.jpg
http://worldoceanreview.com/wp-content/uploads/2013/01/wor2_k2a_s35_massenabfertigung.jpg
Iwapo tutafanikiwa kutekeleza pendekezo hili serikali itakua imefanikisha adhma yake na zaidi kama ifuatavyo:
 1. Itakua imetekeleza sera ya viwanda kwa vitendo na kwa kutumia rasilimali zake kwa maana ya watu, utaalamu, malighafi, na mtaji wa kuanzia ambo tayari umetengwa (million 50 kwa kila kijiji)
 2. Tutakua tumetafutia wanachi wengi ajira. Wako watakaojariwa katika viwanda hivi vidogovidogo, wakaoajiriwa kwa kuzalisha malighafi kama kilimo na kufuga, nk.
 3. Tutafungua fusra za biashara kwa wananchi wataotafuta masoko na kusafirisha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na viwanda hivi ndani nan je ya nchi
 4. Tutakua tumetatua tatizo la ajira na uwezeshaji kwa muda mrefu na kwa wananchi wengi kwa wakati mmoja.
 5. Tutahamasisha sekta binafsi kukua zaidi kwa uanzishwaji wa viwanda vikubwa zaidi vitakavyonunua malighafi kutoka viwanda vidogo
 6. Itahamasisha uimarishaji wa miundombinu vijijini kama barabara, reli, umeme, na maji,  ili kurahisisha usafirishaji wa malighafi na bidhaa pamoja na uzalishaji
 7. Tutapunguza sana gharama ya bidhaa, huduma, na mahitaji mengi
Mapendekezo haya yanaweza kuoneakana kama mageni na yasiyowezekana lakini tukiamua kutumia akili zetu vizuri na kujifunga mkanda kama asemavyo Rais wetu, hakuna cha kutushinda. Kwa mfano,  ni aibu kwamba pamoja na kujisifu kwamba sisi ni nchi ya 2 au 3 kwa wingi wa mifugo Afrika, hadi leo hakuna upatikanaji wa uhakika waziwa masafi na salama na yaliyohifadhiwa na kufungashwa kitaalamu na kupatikana kwenye maduka. Hadi leo tunakunywa maziwa yanayouzwa bila kujulikana yanapotoka, yamewekwa maji, yamechanganywa na mafuta na unga, na yanauzwa kwa bei kubwa sana. Watanzania wengi hawanywi maziwa au vyakula vitokanavyo na maziwa kutokana na ughali, kukosekana uhakika wa usafi na ubora, na ugumu wa upatikanaji. Hatuhitaji utaalamu wowote wa ajabu wa kuhifadhi maziwa vizuri na kuyafanya yapatikane kirahisi.
Katika nchi zilizoendelea na hata zingine zinazofanana na sisi lakini walioamua kuwa serious, wafugaji wengi wana viwanda kidogo mashambani vinavyosaidia kukamua maziwa kisasa zaidi, kuyahidhi kwa usafi, na kuyapack kwenye vyombo na kuyasafirisha kwenda kwa wanunuzi na kwenye maduka. Hata nchi kama ya Kenya walio jirani nasi, wana wafugaji wa aina hii (Tazama mfano wa Kenya hapa: https://www.youtube.com/watch?v=JizSJu4c2mI).
Pili, ni aibu kwamba hadi leo twasafirisha mifugo mamia ya kilometa toka walipo wafugaji kwa lengo la kuja kuichinja Dar es Salaam wakati tungeweza kutengeza machinjio za kisasa na viwanda vya kufanya packaging karibu kabisa na wafugaji.
Ninasisitiza kwamba, kuliko tutumie pesa hizi kuzigawa kwenye vijiji na hatuna hakika ya tija yake, ni nafuu tuanzishe angalau hata kiwanda kimoja kwa kila mkoa au kanda ambacho kitasindika au kuzalisha bidhaa zitokanazo na mazao/malighafi zipatikanazo katika eneo husika.
Imeandikwa na Mwalimu MM


Waweza kumwandikia kupitia [email protected]

 
Toggle Footer
TOP