Loading...
Tuesday

Mwanaume wa miaka 50 Dar ahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kubaka mtoto wa miaka 13

MAHAKAMA ya Ilala jijini Dar es Salaam imemuhukumu Mkazi wa Buguruni, Idd Suma (50) kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 13.

Akitoa hukumu hiyo leo Hakimu Catherine Kihoja alisema ametoa hukumu hiyo baada ya kuridhika na ushaidi uliotolewa mahakamani hapo.

Alisema amepokea ushahidi kutoka kwa Kasudwa Hassan, Khadija Shaha,mtoto aliebakwa pamoja na ushahidi wa pf3 kutoka kituo cha polisi.

Hakimu Kihoja alisema ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Katika utetezi wake Idd alisema anaomba kupunguziwa adhabu kutokana na hali yake ya kiafya si nzuri ikiwa ni pamoja na familia yake inamtegemea.

Wakili wa Serikali Grace Mwanga alisema hanarekodi zozote na mtuhumiwa na kuiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwefundisho kwa watu wenye tabia kama hizo kutokana na matukio hayo kujirudia mara kwa mara.

Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Januari 19 mwaka 2011 majira ya saa 12 jioni katikia eneo la Buguruni kisiwani.
  • Imeandikwa na GLORY CHACKY

0 comments :

Post a Comment

 
Toggle Footer
TOP