Loading...
Saturday

MWR Samia azindua mradi wa ujenzi wa nyumba Palm Villege Msasani Beach Waterfort


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village leo Aprili 09, 2016 unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Group 6 ya China. Mradi huo unaojengwa katika eneo la Msasani Beach Waterfront unategemewa kutoa ajira jumla ya watu 2000 utakapokamilika.

Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea mradi. Kulia Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Jonson Huang

Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Kampuni ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village Msasani Beach Waterfront akikabidhi mfano wa hundi yenye jumla ya Tshs. 10,000,000/= kwa uongozi wa Shule Msingi Mbuyuni kwa ajili ya kuendeleza shule hiyo. Kulia Afisa Muandamizi Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wapili kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Geoge Simbachawene, na Waziri Biasha na Uwekezaji Mhe. Chales Mwijage.

Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi mradi. Kulia Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa China hapa nchini, Guo Haodong. Wa tatu kushoto Mwenyekiti wa Kampuni Uwekezaji ya Group 6, Jonson Huang. Wa pili kushoto ni Mhe. Geoge Simbachawene na Mhe. Chales Mwijage.

Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa pazia kuzindua rasmi mradi.

Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) katika picha ya pamoja na uongozi wa kampuni ya uwekezaji ya Group 6 ya China

Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Guo Haodong
  • Picha na OMR.
 
Toggle Footer
TOP