Nyumba zabomolewa Kibamba; Kaya zaidi ya 30 zakosa makazi

Diwani wa Kata ya Kibamba, Ernest Mgawe akizungumza na baadhi ya wananchi wa mtaa wa Hondogo baada ya nyumba zao kubomolewa. (Picha na Victor Masangu)
NA VICTOR MASANGU, KIBAMBA.

WAKAZI zaidi ya 30 wanaoishi katika mtaa wa Hondogo kata ya Kibamba Wilayani Kiondoni Jijini Dar es Salaam wamejikuta hawana makazi ya kuishi kutokana na nyumba zao kubomolewa bila ya kuzingatia sheria na taratibu kinyume kabisa na haki za binadamu.

Kubomolewa kwa nyumba hizo kumepelekea kwa sasa wananchi hao kuishi katika hali ya sintofahamu kwani nyumba zao walizokuwa wanazitegemea na familia zao zimevunjwa hivyo baadhi yao wameamua kujihifadhi kwa muda kwa majirani zao kutokana na kukubwa na hali hiyo.

Wakizungumza kwa uchungu na katika eneo hilo wakazi hao akiwemo Miriam Mbeleselwa, Ramadhani Kimaro,pamoja na Daima Kimaro walisema kwamba kitendo walichofanyiwa ni cha kinyma na ni ukiukwaji wa haki za binadamu kwani wamevunjiwa nyumba zao bila ya kupewa taarifa yoyote na wamepata hasara kutokana na mali zao nyingi zilizokuwemo ndani kuharibiwa vibaya.

Aidha wananchi hao walisema wamesikitishwa na kitendo kilichofanywa na jeshi la polisi kusimamia zoezi hilo la kuvunja nyumba lifanyike licha ya wananchi hao kuwaonyesha nakala ya hati ya hukumu kutoka mahakama kuu ya adrhi lakini wao walikaidi hukumu ya mahakama na kuamuru kuendelea kuwabomolea wananchi hao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa hondogo Juliasi Sulena alisema kuwa sakata hilo la mgogoro kwa wananchi wa mataa wake analitambua vizuri na kuwa lilishafika katika vyombo husika na limeshafanyiwa kazi na kuongeza kuwa mahaka kuu ya ardhi ilishataoa hukumu kuwa wananchi hao wameshinda kesi.

Nae Diwani wa kata ya Kibamba Ernest Mgawe ambaye alifika kushuhudia athari walizozipata wananchi wa mtaa wa hondongo baada ya kuvunjiwa nyumba ameitaka serikali kuwachukuia hatua kali za kisheria watu wote waliohusika katika kubomoa nyumba hizo.

Mgawe alisema kwamba wananchi hao wa mtaa wa hondogo wameonewa kwani hawakupatiwa taarifa yoyote juu ya kubomolewa nyumba zao , hivyo ameahidi kushirikina nao bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu ili aweze kuona ni namna gani anaweza kuwasaidia.

KUBOMOLEWA kwa nyumba hizo tano katika mtaa wa hondogo kata ya Kibamba Wilayani Kinondoni kumepelekea zaidi ya watu 30 kukosa makazi ya kuishi kutokana na mgogoro huo wa kugombania ardhi ambayo hukumu yake tayari ilishatolewa na mahakama kuwa wananchi hao wameshinda kesi hiyo kihalali.


Diwani wa Kata ya Kibamba Ernest Mgawe akiwaonyesha wananchi wa mtaa wa hondogo barua iliyoandikwa kutoka kwa Kamishina wa ardhi kuhusiana na kushughulikia taratibu zote kwa ajili ya viwanja na sio kubomoa. (Picha na Victor Masangu)

Baadhi ya wakazi wa eneo hio la mtaa wa hondogo wamekiwa wameketi chini wakijadiliana jambo baada ya nyumba zao kubomolewa bila ya kuzingatia sheria na taratibu kwa madai walivamia eneo ambalo lilikuwa linammiiki wake wakati eneo hilo wameinunua kihalali.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo la mtaa wa hondogo kata ya Kibamba akielezea kwa uchungu kwa waandishi wa habari waliofika katika eneo hili kushuhudia baadhi ya nyumba zilizobomolewa bila ya kufuata utaratibu wowote wa kiserikali.(Picha na Victor Masangu)
---