Loading...
Wednesday

Taarifa ya SUA: Kujiunga na NHIF na Majina yaliyowasilishwa

UFAFANUZI KUHUSU TANGAZO LA USAJILI KATIKA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF) 

Tunapenda kutoa ufafanuzi kuwa, ni kweli zoezi la usajili katika Mfuko wa “NHIF” lilianza tarehe 18 Januari, 2016 na lilipaswa kumalizika tarehe 31 Januari, 2016. Hata hivyo zoezi hilo halijakamilika kama ilivyokuwa imepangwa. Aidha, kumejitokeza changamoto hususan kuhusu aina ya wategemezi kwani wafanyakazi wengi wamekuwa hawakubaliani na maelezo wanayopewa na Maafisa wa Chuo wanaoshughulika na zoezi hili na hivyo kusababisha ugumu wa kiutekelezaji. Kufuatia hatua hiyo ikaonekana ni vyema kuwaita “NHIF” kwa ajili ya kuwaelimisha wafanyakazi na hivyo kurahisisha zoezi. 

Ujio wa maafisa wa ”NHIF” hauwahusu wafanyakazi ambao fomu zao zimekwishawasilishwa Utawala, zikasainiwa na kupelekwa “NHIF” kwa hatua zaidi. Wafanyakazi ambao majina yao yamo katika orodha iliyoambatanishwa na wale ambao tayari wamekwishasajiliwa na kupewa vitambulisho hawahusiki na zoezi hili. 

Samahani kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

  • Wafanyakazi wafuatao wanaombwa kuchukua kadi zao za uanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii mlango na. 218 jengo kuu la utawala. Bofya hapa kuona majina

 
Toggle Footer
TOP