Loading...
Sunday

Taarifa ya Wizara kuhusu maonesho ya kimataifa ya madini ya vito ArushaWizara ya Nishati na Madini (MEM) kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA), wanawaalika wadau wote wa Sekta ya Madini na wamiliki wa Leseni ya Biashara za Madini, Masonara na Wachimbaji wa Madini ya Vito kushiriki kwenye Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Madini ya Vito Arusha (Arusha Gem Fair - AGF).

Maonesho haya yatafanyika katika Hoteli ya Mount Meru ya Arusha, kuanzia tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016.

Maonesho ya AGF kwa mwaka 2016 yanalenga kuendeleza azma ya kuifanya Arusha kuwa kituo Kikubwa cha madini ya vito Afrika. Pia, maonesho haya yatawakutanisha washiriki (exhibitors) zaidi ya 100 kutoka nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini na wanunuzi wa kimataifa zaidi ya 500 pamoja na wadau mahiri wa tasnia ya vito. Maonesho pia yanadhamiria kuendeleza biashara ya madini ya vito katika nchi za Mashariki, Kati na Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kutokana na hilo, Wizara ya Nishati na Madini haitatoa vibali vyovyote vya kusafirisha madini ya vito nje ya nchi kuanzia tarehe 5 hadi 28 Aprili, 2016. Ili kuhakikisha kuwa kunakuwepo na madini ya vito ya kutosha kwenye maonesho haya.

Vibali vitatolewa kwa Washiriki wa maonesho pekee kuanzia tarehe 19 Aprili, 2016 hadi maonesho yatakapokwisha. Lengo letu ni kuhakikisha maonesho haya yanafanikiwa na kuifanya Tanzania kuwa kituo kikubwa cha biashara ya madini ya vito barani Africa.
Mabanda ya maonesho yanapatikana kwa gharama za Dola za Marekani 1,000. Kamati ya Maonesho inasimamia ugawaji wa mabanda hayo kwa ushindani (first come-first be served).

Taarifa kuhusu usajili zinapatikana katika Ofisi za Madini za Kanda zilizo katika Miji ya Arusha, Mwanza, Dar es salaam, Mtwara, Mpanda, Shinyanga, Mbeya, Musoma, Songea na Singida au Ofisi za TAMIDA.

Wanunuzi wanatakiwa kujisajili kupitia tovuti ya maonesho: www.arushagemshow.com;
au kwa barua pepe ya maonesho: [email protected] ; au kwa njia ya simu zifuatazo +255 784352299 or +225 767106773.

Imetolewa na,
Katibu Mkuu
 
Toggle Footer
TOP