Loading...
Monday

"Wanaliita lile daraja - Daraja la Dau"

null
Dk Ramadhani Dau na Mohammed Said
Katika upande wa akili Allah kamjaalia akili ambayo si ya kawaida. Yeye siku zote kuanzia darasa la kwanza hadi Chuo Kikuu namba yake ni moja. Ziko sifa zake nyingi lakini kwa leo tutosheke kwa haya. Twende kwenye Daraja la Kigamboni. Watu wa Dar es Salaam wanaliita Daraja la Dau. Siku moja nilikuwa nazungumza na Dr. Dau nikamuuliza daraja linakwendaje? Hapo ndipo nikamwambia kuwa kwingi ninapopita Kariakoo jamaa wanaliita lile daraja - Daraja la Dau. Dr. Dau akatingisha kichwa akacheka.

Daraja la Dau leo limekuwa kweli. Daraja limekamilika kujengwa na leo magari yameanza kupita. Wananchi wamefurahi na picha nyingi zimepigwa na watu waliotumia daraja hilo leo. Baada ya miaka mingi ya foleni zinazochosha leo hii barabara ya kuingia Ferry kuvuka kwenda Kigamboni ilikuwa nyeupe.

Hili ni Daraja la Kigamboni. Lakini itakapokuja kuandikwa historia ya daraja hili jina la Dr. Ramadhani Kitwana Dau litaandikwa pamoja na historia ya daraja na historia nzima ya Kigamboni na Dar es Salaam yake. Hao watakaokuja baada yetu ndiyo watakuwa waamuzi waadilifu wataosimama katikakati ya mizani na kumpima ndugu yangu Ramadhani kwa mizani iliyo sawa.

Jisomee makala nzima ya Mohammed Said kwenye blogu yake akimwelezea Dk Ramadhan Dau kwa kubofya hapa.
 
Toggle Footer
TOP