Loading...
Thursday

Zitto Kabwe afanya kikao na Watanzania wanaoishi New York


Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini akisisitiza jambo mbele ya vijana wa Kitanzania waishio New York.

Zitto alipata nafasi ya kuongea na vijana hao waliotaka kujua maendeleo ya nchi yao na changamoto zake ndani ya bunge la Jamhuri anavyowakilisha hoja zake kwa faida ya wananchi kupitia upinzani, pia yeye kama mwanasiasa aliye upande wa upinzani, mtazamo wake juu ya kasi ya rais wa wamu ya tano, John Pombe Magufuli.

Zitto yupo New York City kwa kivuli cha World Bank na pia alipata nafasi ya kutembelea Columbia University New York na kuongea na wasomi wa huko. Pia atapata nafasi ya kutembelea Harvard University huko Boston, MA.

  • Picha zote na maelezo, tumeshirikishwa na Vijimambo Blog, New YorkZitto akipata ukodak baada ya kukutana na Watanzania New York City. Kwa taswira zaidi nenda soma zaidi.

Zitto akitafakari swali kabla kujibu, Zitto aliulizwa kama yupo tayari kuungana na Ukawa na kama yupo tayari kungombea kiti cha urais kupitia chama chake ACT, majibu yalikuwa yupo tayari kuungana na ukawa lakini anaitaji kujua nini faida ya kuungana na kama kuungana ili kuing'oa CCM basi iwe na nguvu kweli kweli na ifanikiwe kwani asinge penda kuungana na nakubakia msindikizaji tu bila faida endelevu na kama yupo tayari kugombea kiti cha urais basi atafanya hivyo akiwa amesha jiandaa vilivyo ili akigombea apata ushindi wa kishimdo na kuing'oa CCM na siyo vinginevyo.
Hapa ni Rakesh Rajani akiuliza swali kwa Zitto. Rajesh ni Mtanzania mwenye asili ya India ambaye aliandaa mkutano huu kwa kushirikiana na Nathan Chiume.

Shabani Mseba akiuliza swali kwa Zitto kuhusu mipango maendeleo jimboni kwake.

Zitto alieleza mipango ya kuhakikisha elimu inakuwa na mwamko ndani ya mkoa wake kutokana na ufaulu kushuka.


 
Toggle Footer
TOP