DC Kinondoni awaagiza wenyeviti wa mitaa kuwatangaza wakazi wachafu


Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Ally Hapi amewaagiza wenyeviti wa serikali za mitaa wilayani humo kuwatangaza na kubandika picha za wakazi wote watakaoshindwa kufanya usafi katika maeneo yao.

Hapi ameyasema hayo wakati wa zoezi la ufanyaji usafi na kupanda miti katika kata ya Sinza A, zoezi lililoendeshwa na kikundi cha wanawake wa millenia.

Wakizungumza kabla ya upandaji miti, wanawake wa milenia wameshauri mitandao ya kijamii itumike kuhamasisha masuala mbalimbali ya utunzaji wa mazingira.

Naye mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni amesema manispaa itaweka vizimba vya kukusanya taka, hivyo watu wasisite kufanya usafi.