Loading...
Sunday

Hii inawezekana Marekani tu! Jamaa "akomoa" kwa kulipa tiketi 'ya trafiki' $212 kwa sarafu za senti 10

Jamaa akimwaga sarafu kaunta
Jamaa mmoja nchini Marekani katika jimbo la Texas aliyepinga kupewa tiketi kwa kuendesha gari kwa mwendo zaidi ya unaoruhusiwa, ametii amri ya hakimu kwa staili aliyoichagua yeye, ili kuonesha hasira yake.

Jama huyo alitakiwa kulipa dola za Kimarekani $212 lakini kwa kuwa unapaswa kulipa bila kujali aina ya ulipaji wa fedha hizo, jamaa huyo aliamua kuomba chenji kwenye benki, akataka sarafu za kiwango cha chini kabisa cha fedha.

Alipopata sarafu zake, akaingia katika karakana, akabadili ndoo mbili nyeupe kwa kuzipaka rangi nyeusi na kisha kuandika maneno ya kejeli kabla ya kuchukua beleshi na kuzisunda ndani na kisha kuzibeba hadi dirisha la malipo na kuzibwaga kwenye kaunta ya dirisha hilo, huku akiwaeleza wahudumu kuwa wanaweza kumtumia risiti kwa kutumia anwani yake kwa kuwa wanayo na kama kuna ziada wanakaribishwa kuihifadhi kwa ajili ya matumizi yao.


Iliwachukua mwendo wa saa tatu wahudumu kuhesabu safaru hizo katika mashine na kugundua kuwa jamaa aliwaachia ziada ya $7 hivi.

Kosa lenyewe ni la kuendesha katika mwendo wa maili 39 kwa saa katika eneo linaloruhusiwa kuendesha maili 30 tu kwa saa.

 
Toggle Footer
TOP