Loading...
Monday

Maazimio ya KUB: Kujalidi agenda 2: Kutokuwa na imani na NS, Tulia Ackson; Kutoka nje kila awapo

UPDATE: Mei 31, 2016


Wabunge wa vyama vya upinzani leo wametoka nje kwa mara nyingine kupinga Naibu Spika Dk. TuliaAckson kuendesha vikao vya Bunge na kumwachia Bunge yeye na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Taarifa kutoka Bungeni zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Dk Tulia.

Baada tu ya kusomwa dua ya kufungua Bunge asubuhi wabunge hao wametoka nje na kumwacha Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee.

Hata hivyo Dk. Tulia ameanza kupaniwa na wapinzani tangu jana. Ni kwa madai kuwa wapinzani hawamwamini tena.

Wameeleza kuwa, namna anavyoliongoza Bunge, kauli zake na kuyumba kwake katika kusimamia haki kwa wabunge wa Ukawa na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumechochea kuonekana kuwa, nafasi aliyonayo haimstahili.

Kutokana na hali hiyo, Freeman Mbowe ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni jana aliahidi kuanzisha mgomo dhidi ya Dk. Tulia.

Mbowe aliwaambia hayo wabunge wenzake mjini Dodoma kwenye kikao cha dharura alichoitisha na kushirikisha waandishi wa habari.

Alisema, Dk. Tulia ndio tatizo kuu la Bunge la Kumi na Moja na kwamba, kiongozi huyo wa Bunge kila anapokuwa kwenye kiti na kuongoza Bunge, mtafaruku hutokea.

“Nitapendekeza kuwa kila kikao cha Bunge kinachoongozwa na Tulia Ackson, sote tutoke nje ili kuonesha kwamba hatuna imani naye katika kuendesha shuguli za bunge,” Mbowe alisema jana.

Utekelezwaji wa kauli ya Mbowe umeanza leo ambapo sasa Dk. Tulia amebaki na wabunge wa CCM pekee.


Kutokana na kilichotokea Bungeni leo, Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (Mb) amekutana na wanahabari kwa ajili ya kufikisha maazimio ya kambi hiyo kwa umma kuwa, watajadili agenda mbili, mosi ikiwa ni ya kutokuwa na imani na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bi Tulia Ackson na pili, kutoka nje ya ukumbi wa vikao vya Bunge kila Naibu Spika huyo awapo, ikiwa ni hatu ya kuonesha kutokukubaliana na namna Bunge hilo linavyondeshwa kwa kile walichokiita, kuogonzwa na mtu asiyefahamu au kwa kupokea maagizo kutoka kwingine.
 
Toggle Footer
TOP