Loading...
Sunday

Meya wa Ilala ataka nyumba za wageni ziwe na CCTV camera

Kufuatia matukio kadhaa ya uhalifu ikiwemo mauaji yanayofanywa katika nyumba za kulala wageni, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amependekeza ufungwaji wa kamera maalum za Closed-Circuit Television (CCTV) katika nyumba hizo ili kuimarisha ulinzi.

Amesema mamlaka husika wakiwemo wamiliki wa gesti na hoteli wanapaswa kuliangalia suala hilo kwa jicho la tatu ikiwa ni siku chache zimepita tangu kuripotiwa tukio la kufariki mwanamke mmoja akiwa gesti Jijini Dar es Salaam.

“Kamera hizi hazitafungwa vyumbani bali zifungwe maeneo ya nje ya gesti au hoteli husika, mapokezi kwani hii ndio itakuwa njia sahihi ya kupambana na matukio ya kihalifu kama haya na kuwabaini wahalifu,” ameongeza Meya Mwita.

Amewataka pia viongozi wa dini wa Mkoa wa Dar es Salaam kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili wakazi wa Jiji hilo waweze kumrudia Mungu na kuachana na vitendo vya kinyama.

Wakati huohuo, Meya Mwita amekanusha vikali taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamiii kuwa ameagiza wamiliki wa gesti na hoteli kuwapiga picha wageni wanaokwenda kulala katika nyumba hizo.

0 comments :

Post a Comment

 
Toggle Footer
TOP