Mgomo UDSM "kimeeleweka" cheki imetoka

Wanafunzi UDSM katika mgomo leo
Kwa mujibu wa gazeti la MwanaHALISI Online, leo Mei 31, 2016 Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) waligoma kusitisha mgomo wao mpaka pale pesa za kujikimu zitakapoingizwa kwenye akaunti zao.

Mgomo huo ulianzishwa baada ya kucheleweshwa fedha zao za kujikimu zinazotolewa kila baada ya siku 60.

Wanafunzi hao walikuwa wakidai fedha hizo baada ya kupita siku tano bila kupewa taarifa yoyote ikiwemo kwamba, serikali haina fedha.

Mgomo huo ulianza saa mbili asubuhi na kuendelea hadi mchana kwa ahadi ya kutokukoma kutokana na msimamo wa wanafunzi hao wa kutoacha kugoma mpaka watakapopatiwa haki yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Prof. Rwekaza Mkandara, Makamu Mkuu wa UDSM amesema kuwa, fedha hizo zingetolewa kabla ya kufuka Saa 12 jioni.

Awali msimo wa wasomi hao ulimtaka Paul Makonda (Mkuu wa Dar es Salaam), Ally Salum Hapi, (Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni) na Boniface Jacob (Meya wa Manispaa ya Kinondoni), kuzungumza nao.

Erasmi Leon, Rais wa Serikali ya Wanafunzi UDSM na Mshangama Shamira, makamu wake wamesema kuwa, mgomo husika utaendelea mpaka pale watakapothibitisha kuwa, fedha zao zimeingia katika akaunti zao.

Wanafunzi walikusanyika katika eneo la Revolution Square lililopo chuoni hapo kwa amani huku wakiimba nyimbo mbalimbali za uzalendo.

“Kama sio juhudi zako Nyerere…, Sitasimama maovu yakitawala…., Vijana tusilale bado mapambano…. alisema Nyerere vijana wote tumelegea sharti tuanze mchakamchaka….” Wamesikika wakiimba.

Mpaka mchana unaisha, viongozi waliowahitaji kuzungumza nao hawakuwa wemefika kwenye eneo hilo.


  • UPDATE: wavuti. imepata picha kupitia WhatsApp kwa maeleo kuwa ni nakala ya idhini halisi ya malipo ya madai ya wanachuo hao, iliyotolewa leo.