Loading...
Monday

Njau: Mfumo wa usimamizi wa mabasi ya haraka Dar uwe kigezo kwa daladala

Nimefurahishwa sana mfumo wa usimamizi wa mabasi ya mwendo kasi Jijini Dar es salaam ambao unajali muda wa abiria kuwahi kwenda na kurudi katika shughuli za kiuchumi na kijamii pia.

Mfumo huu unawezekana kwa mabasi daladala katika ruti zote Jijini kuachana na ule mtindo wa kulala vituoni kusubiri abiria huku wakiwachelewesha abiria ambao wameshapanda kwenye mabasi husika.

Sumatra kwa kushirikiana na wamiliki wa daladala,mamlaka za Manispaa,Jiji na kikosi cha usalama barabarani wakutane kwenye meza ya mviringo kwa ajli kubuni mfumo wa usimamizi na uendeshaji wenye tija kwa wadau na Taifa kwa ujumla.

Inasikitisha sana hasa nyakati za asubuhi na jioni kuona abiria wamejaza kwenye vituo vya mabasi wakiwa na hawana mwelekeo lakini wakati huohuo mabasi ya daladala yapo kwenye vituo vikuu vya mwanzo au mwisho wa ruti wakipiga na debe na kupakia abiria kwa kufuata foleni na kugoma kuondoka hadi abiria wajazane na kwenye viti na kusimama.

---
Ray Njau
 
Toggle Footer
TOP