Loading...
Friday

Taarifa ya TRA ya makusanyo ya kodi kwa mwezi Aprili 2016 na mpango wa kugawa bure EFDs

Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari (Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO)
Na Lilian Lundo MAELEZO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imejipanga kugawa jumla ya mashine 5700 za (Electronic Fiscal Devices) EFDs kwa wafanyabiashara wadogo wadogo nchini ikiwa ni jitihada za Serikali katika kukusanya mapato nchini.

Akizungumzia mipango hiyo leo, Jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata amesema wameamua kuanza kugawa mashine hizo kwa wafanyabiashara wadogowadogo ambao wengi wao hawana uwezo wa kugharamia manunuzi ya mashine hizo.

“ Mamlaka imeona changamoto wanayoipata wafanyabiashara wadogo hivyo imeamua kuanza kugawa mashine hizi ili kuondokana na tatizo la kutotoa risiti za mauzo kwa wafanyabiashara hao ambao walio wengi walikuwa na kisingizio cha kutokuwa na mashine hizo”. Alisema Kidata.

Kamishna Kidata ameongeza kuwa Mamlaka yake imeshaagiza mashine hizo na zipo tayari kuanza kugawiwa mwezi huu kwa wafanyabiashara hao ikiwa ni awamu ya kwanza ya ugawagaji wa mashine hizo ambao utafanyika nchi nzima.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeazimia kugawa mashine laki mbili kwa wafanyabiashara wadogo wadogo nchini ikiwa ni jitihada za kuweza kukusanya mapato yatokanayo na kodi za biashara kwa urahisi na ufanisi mkubwa.

0 comments :

Post a Comment

 
Toggle Footer
TOP