Loading...
Tuesday

Tahadhari kutoka Bagamoyo kwa wanaokwenda kununua maeneo ya ardhi

TAHADHARI KUTOKA BAGAMOYO

Ukija Bagamoyo kununua kiwanja au shamba, usikumbuke kuja na hela yako peke yake, bali pia kumbuka kuja na AKILI ZAKO! Bila hivyo UTABAMBIKIWA HIVI:-
 1. SHAMBA AU KIWANJA FEKI.
 2. MWENYEKITI wa Kijiji FEKI.
 3. AFISA MTENDAJI wa Kijiji FEKI.
 4. MUUZAJI wa Kiwanja/Shamba FEKI.
 5. SHAHIDI FEKI.
 6. JIRANI anayejifanya ndio anapakana na kiwanja au shamba unalouziwa, FEKI.
 7. WATOTO FEKI - wataitwa kuchezacheza ili muuzaji aonekane ana familia na si mhuni.
 8. MKE wa muuzaji, kwamba ataitwa kukusalimia - FEKI
 9. NYARAKA FEKI 
 10. MIHURI FEKI
 11. OFISI ya Kijiji FEKI - bendera ya taifa itawekwa nje ya ofisi kama boshen.
 12. Siku ukigundua umeuziwa kiwanja cha mtu au shamba lililoko katika mradi wa EPZA, hao wahusika wote huwaoni na ndipo utagundua kuwa hata namba zao za simu ni FEKI.
Kuweni makini, kwani ukishapigwa hela zako za mkopo wa BAYPORT/CRDB/AMANA BANK/ACCESS BANK, PSPF, LAPF, PPF na nani mwingine sijui, fahamu kuwa vitisho vya Polisi au kuwaroga, havitasaidia. Hawa jamaa kwa jinsi walivyo smart,hutawapata kwa polisi na wala hawarogeki. 

USIJE UKASEMA ULIKUWA HUJUI! NIMEKUKANYA.

TAHADHARI KABLA YA HATARI.

-------
via WhatsApp
 
Toggle Footer
TOP