Loading...
Tuesday

Tanga: Ahukumiwa kwenda jela mwaka 1 kwa kuuza kitoweo cha nyama ya mbwa

Mtuhumiwa na kithibitisho
Kijana Mmoja aliyejulikana kwa jina la Zakaria Mswaki mkazi wa Mlalo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga amehukumiwa na mahakama ya mwanzo Mlalo Wilayani humo kifungo cha mwaka mmoja jela kwa tuhuma za kukutwa akiuza nyama ya mbwa.

Tukio hilo limetokea hivi karibuni ambapo asilimia kubwa ya watu katika mji huo mdogo uliopo katika Wilaya hiyo walinunua nyama hiyo na kula bila kujua ambapo mshtakiwa alikiri shitaka hilo mbele ya mahakama hiyo.

Mshtakiwa huyo alidai chanzo cha kujihusisha na biashara hiyo haramu ni kutokana na ugumu wa maisha unaomkabili kwa kipindi kirefu sasa hali iliyompelekea kujiingiza katika biashara hiyo.

Mshtakiwa huyo alikiri shitaka hilo mbele ya mahakama na kudai ugumu wa maisha ndio chanzo cha yeye kufanya biashara hiyo.

Sambamba na hayo Mshtakiwa huyo alipelekwa gerezani Wilayani humo kwa ajili ya kutumikia adhabu yake huku akiwaacha wananchi wa mji huo na butwaa na hasira kwa kulishwa nyama ya mbwa.
 
Toggle Footer
TOP