Loading...
Sunday

TRA yagawa bure sukari iliyokamatwa

Richard Kayombo
Richard Kayombo
Mamlaka ya mapato nchini TRA mkoa wa Lindi imegawa sukari iliyokamatwa kwa njia ya magendo mifuko 5,319 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 73 kwa taasisi 31 mkoani humo baada ya TFDA kuthibitisha kuwa sukari iko salama kwa matumizi ya binadamu.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa sukari hiyo, Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA Richard Kayombo amesema baada ya kukamatwa kwa bidhaa hizo, TRA kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, iliamuliwa sukari hiyo kuigawa kwa watu wenye uhitaji katika mkoa huo zikiwemo taasisi za elimu, afya, kambi za wazee na jeshi la magereza.

Sukari hiyo ilikamatwa mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi ikiingizwa nchini kinyume cha sheria kutoka nchini Brazil kupitia bandari ya Zanzibar.

Kayombo ametoa wito kwa wanaofanyabiashara za magendo na ukwepaji kodi kuacha kwani TRA imejipanga kudhibiti biashara hizo.
  • Taarifa ya TBC

 
Toggle Footer
TOP