Loading...
Monday

Wimbo na Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Utaratibu wa matumizi

TAARIFA KWA UMMA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kutoa utaratibu wa matumizi ya Bendera na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kama ilivyotangazwa hivi karibuni.

Utaratibu huo ni kwamba Bendera ya Taifa itaanza kupeperushwa ikifuatiwa na Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, vivyo hivyo Wimbo wa Taifa utaanza kupigwa ukifuatiwa na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilitatangaza kuhusu matumizi ya Bendera na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Wizara, Idara, Mashirika na Taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na Taasisi Binafsi.

Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unapatikana katika tovuti ya Wizara ambayo ni www.foreign.go.tz.

Aidha, kwa mujibu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki vipimo maalum vya kutengeneza Bendera hiyo ni kama vinavyoonekana hapa chini.Imetolewa na,
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 23 Mei, 2016.
 
Toggle Footer
TOP