Loading...
Tuesday

Watanzania 408 wanatumikia vifungo nchi za nje kwa kusafirisha dawa za kulevya

Watanzania 408 wanatumikia vifungo nje ya nchi na wengine kukabiliwa na adhabu ya kifo baada ya kusafirisha dawa za kulevya.

Taarifa hiyo imetolewa bungeni leo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga alipokuwa akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Akizungumzia Watanzania waliokamatwa kwa dawa hizo Mahiga amesema wanakabiliwa na adhabu hizo katika magereza mbalimbali duniani baada ya kukutwa na hatia ya makosa ya kujihusisha na biashara haramu.

Mahinga alitaja idadi yao na nchi ambazo wanashikiliwa kuwa ni Brazil (41), China (266), Iran (68), India (9), Nepal (4), Oman(3), Thailand (14) na Umoja wa Falme za Kiarabu (3). [MWANANCHI]
 
Toggle Footer
TOP