Loading...
Tuesday

Askari walivyosambaratisha wanachama na wafuasi wa CHADEMA Shinyanga

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wamewasambaratisha viongozi, wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ), waliokuwa wamehudhuria katika mkutano wa uzinduzi wa ‘Operesheni okoa Demokrasia’ katika uwanja wa CDT mjini humo kwa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.


Askari hao walianza kufyatua mabomu ya kutoa machozi na kumwaga maji ya kuwasha kuanzia majira ya 9 alasiri, huku baadhi ya wananchi nao wakijihami kwa kurusha mawe, ambapo vurugu hizo zilidumu kwa zaidi ya saa moja na kusababisha maduka kufungwa, huduma za usafiri kusimama na baadhi ya wakazi wa maeneo yaliyopo jirani na uwanja huo wa CDT kujifungia ndani kutokana na moshi wa mabomu huku jamaa za wagonjwa waliolazwa katika zahanati ya Kahama Community wakilalamikia hali hiyo.

Zaidi ya watu 20 wakazi wa mji wa Kahama, akiwemo mratibu wa CHADEMA kanda ya Serengeti Renatus Nzemo wanashikiliwa na jeshi la polisi katika vurugu hizo za kuzima mkutano wa CHADEMA, ambao ulikuwa umehudhuriwa na wabunge saba wa chama, viongozi waandamizi wa chadema ngazi ya Taifa na kanda wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Mh. Freeman Mbowe.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jioni la leo na Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Nsato Mssanzya amepiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara hadi hali ya usalama itakapotengemaa.

Amesema Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu yoyote au chama chochote kitakachokaidi agizo hilo.


Baadhi ya wafasi wa cha ma hicho wakiwa na mabango nyenye maneno ya kuikejeli serikali ya ccm kwa kutumia jeshi la polisi kwa kudhibiti madamano hayo .

KAHAMA:

JITIHADA za Jeshi la Polisi nchini kudhibiti kwa amani maandamano yasiyo na kikomo ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupinga kuendelea kwa bunge la Katiba imeshindikana wilayani Kahama baada ya kuwatanya wafuasi wa chama hicho kwa mabomu.

Maandamano hayo ambayo yanaratibiwa nchi nzima na chama hicho ambapo maeneo mbalimbali nchini yalishindikana kufanyika zaidi ya kuonekana Askari Polisi wakirandaranda mitaani,wilayani Kahama chama hicho kimethubutu kuyafanya,na kulifanya Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga kuyadhibiti kwa kupiga mabomu ya machozi.

Katika maandamano hayo ambayo kulikuwa na wafuasi wengi wa chama hicho waliokusanyika katika ofisi za wilaya za chama hicho kuanzia saa moja asubuhi yakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Juma Protas na baadhi ya madiwani wa chama hicho wakiwa wamejifunga vitambaa vyeupe mikononi mwao kuashiria amani.

Wafuasi hao waliokuwa na mabango mbalimbali yanayolaani seriakali mabango hayo miiongoni yakisomeka; “Serikali ya CCM inachofanya ni utapeli mtupu.Bunge la Katiba ni mpango wa wizi mtupu ole wenu 2015.”pia “Kikwete ,Samweli 6 Ufedhuli wa kufuja fedha za Watanzania kwa kigezo cha Bunge la Katiba acheni mara moja”na mengine kibao,walianza maandamano hayo rasmi mnamo saa tatu asubuhi.

Wakiwa katika maandamano ambayo yalitawaliwa na utulivu wakianzia katika ofisi zao za chama wakiwa na vitambaa vyeupe walivyovaa kichwani na mikononi ghafla ziliibuka gari nne za polisi zilizokuwa na askari zikiongozwa na PT 0841,walifika na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi wafuasi hao,hatua ilileta mparanganyiko mkubwa.

Aidha baada ya Polisi hao kuwatawanya kwa mabomu wafuasi hao wa CHADEMA walifanikiwa kuwatia mbaroni viongozi watatu wa Chama hicho ambao ni Mwenyekiti wa wilaya,Juma Protas,Diwani wa Kata ya Nyihogo,Amosi Sipemba na Diwani viti maalumu Winfrida Mwinula.

Hata hivyo baada ya kukamatwa Mwenyekiti wa Chama hicho alisema Bunge la Katiba kusimamishwa mara moja kinachofanyika Dodoma hakiwezi kupelekea kupata Katiba ya Watanzania.

Alilaani kitendo cha kukamatwa na polisi waliotumia nguvu kuwatawanya kwa silaha watu ambao hawakuwa na silaha wala kuashiria uvunjifu wa amani,huku akisisitiza kuwa serikali imepiga marufuku maandamano kwa ujumla wake lakini uongozi wa chama chake wilaya uliandika barua ya kutoa taarifa kwa mujibu kanuni na sheria ya vyama vya siasa.

“Katiba inaturuhusu kutoa taarifa kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza,hatua ambayo tuliietekeleza lakini Jeshi la Polisi halikutoa majibu kama limeyazuia maandamano hayo”,Alisema Protas.

Alisema anashangazwa na Jeshi hilo kuleta askari wengi wakiwa za moto na mabomu ya mchozi na magari manne jambo ambalo lingeweza kujibiwa kwa maombi ya barua tuliyowapelekea.

Naye Diwani wa Viti Maalumu Winifrida Mwinula alisema kuwa Bunge hilo linaendelea kula fedha za wananchi jambo ambalo mbunge mmoja katika Bunge la Katiba analipwa shilingi Laki saba kwa siku jambo ambalo mwananchi wa kawaida anashindia mlo mmoja duni kwa siku huku wao wakiendelea kuneemeka huku wananchi wa kawaida wakiwa na maisha duni.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nyihogo Amosi Sipemba alisema kuwa jambo la maandamano lilpo kikatiba na Chadema wanachokiona katika Bunge la Katiba halina manufaa kwa wananchi hasa kwakuwa linapindishwa pindishwa na kuona kinachofanyika ni ufisadi mtupu.

Pia mfuasi mmoja wa chama hicho Injinia Tadeo Joachimu alisema kuwa inashangaza jeshi la polisi kuyaingilia wakati yapo Kikatiba,na kukilaani chama cha mapinduzi kutumia dola kukiangamiza CHADEMA jambo ambalo alidai ukiukwaji wa Katiba.

MATUKO KATIKA PICHA:


Hivi ndiyo hali ilivyokuwa katika mji wa kahama wakati wa mandamano ya chadema ambapo jeshi la polisi limewenza kuzibithi madamano hayo .

Gari la polisi likiwa katika doria la kudhibiti mandamano hayo .

Hivi ndiyo wanachama wa chama cha maendeleo chadema katika ofisi yao.

Haya ndiyo mabango yalikuwa yameshikwa na wafasi wa chama hicho .

Hii ndiyo ofisi ya chadema wilaya ya kahama .

Mmoja wa wanachama wa chadema Eng Thadeo Joackim mwenye suti nyeusi akiwa katika ofisi ya chama hicho baada ya kudhibitiwa kwa mandamano hayo.

Hivi ndiyo wafasi wa chama hicho wakiwa na mushangao wa kuzuhiwa kwa mandamano hayo leo mchana.

Umati wa wanachama wa chadema wakiwa ofisini kwao wakitafakali hali ya kuzuiwa kwa madamano hayo. .

Jeshi la polisi wilayani kahama likiwatawanya baadhi ya wanachama wa chadema leo mchana katika barabara ya samanga.

Diwani wa viti maalumu wa chadema Winnefrida mwanula akiwa katika kituo cha polisi wilani kahama baada ya kukamatwa jeshi hilo kwa kuvunja amri halali ya jeshi la polisi .

Mwenyekiti wa chama cha maendeleo chadema juma Protes akiwa na baadhi ya madiwani wa chama hicho winnefrida mwenula mwenye kofia na Amosi sipemba wakiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi baada ya kukamatwa wakati wakihitisha kwa mandamano hayo.

Mwenyekiti wa chadema wilaya ya kahama juma Protes akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi leo mchana baada ya jeshi hilo kudhibiti kwa mandamano hayo .

Baadhi ya wafasi wa chama hicho wakiwa nje ya ofisi hiyo .mwenye suti Eng Thadeo jockimu akiwa ameshika kitabaa cheupe kwa kuashilia Amani kwenye madamano hayo .

Haya ndiyo mabango yaliondikwa na wafasi wa chama hicho.

Mwenyekiti wa chadema wilaya ya kahama juma Protas akiwa juu ya jukwaa la Mkutano wa chama hicho kabla ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho.

Baadhi ya wanachama na wafasi wa chama hicho wakiwa katika viwanja vya CDT wakisubiri viongozi wa kitaifa kuwasili katika viwanja hivyo

Waandishi wa habari wa Vyombo mbali mbali wakiwa katika uwanja wa CDT wakisubiri mkutano wa CHADEMA

ANGALIA MATUKIO YA PICHA UWANJA WA CDT MJINI KAHAMA

KAHAMA

JESHI la Polisi Wilayani Kahama kwa kushirikiana na lile la Mkoani Shinyanga jana limeweza kuwasambaratisha kwa kutumia mabomu ya Machozi na gari la maji ya washa wafuasi na Viongozi wa Juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wakitaka kufanya mkutano mjini hapa kinyume cha Sheria.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa saba za mchana katika kiwanja cha CDT kilichopo mjini hapa wakati viongozi hao wa ngazi za juu wa Chama hicho waliopokuwa wakitaka kufanya mkutano wa kufungua kampeni ya operesheni "Okoa Demokrasia" kanda ya ziwa.
 
Toggle Footer
TOP