Loading...
Thursday

Rais Magufuli aweka jiwe la msingi la maktaba UDSM; Azungumzia agizo la kuondoa wanafunzi 7802 UDom

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali yake ya awamu ya tano itahakikisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanapatiwa mikopo, lakini haitakubali kulekeza mikopo hiyo kwa wanafunzi wasiokuwa na sifa za kujiunga na vyuo vikuu.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 02 Juni, 2016 wakati akizungumza na Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa maktaba ya kisasa ya chuo hicho inayojengwa katika kampasi ya Mlimani upande wa mashariki mwa chuo.

Akiwahutubia maelfu ya wanajumuiya hiyo wanaojumuisha wanafunzi, wahadhiri na wafanyakazi wa chuo, Dkt. Magufuli amesema serikali yake imedharia kutoa elimu bora kwa watanzania na imejipanga kuhakikisha inakabiliana na changamoto mbalimbali zinazovikabili vyuo, lakini ameelezea kusikitishwa kwake na uwepo wa wanafunzi waliodahiliwa na baadhi ya vyuo hapa nchini pasipo kuwa na sifa zinazomwezesha mwanafunzi kujiunga na chuo kikuu.

"Wapo wanaokopeshwa mikopo hii ya elimu ya juu lakini hawana sifa, Mheshimiwa Profesa Ndalichako (Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi) nakushukuru kwa hatua unazozichukua katika kusafisha wizara yako na hili nalisema kwa uwazi, na ukweli lazima usemwe hata kama ni mbele ya wanachuo.

"Una D,D unasajiliwa kuchukua digrii chuo kikuu na unapata mkopo wa serikali, ni aibu ya ajabu, haiwezekani, haiwezekani, haiwezekani. Lakini wakati tunawalipia wanafunzi 489 waliomaliza kidato cha nne na kupata D,D manaake wengine ni divisheni 4, kuchukua digrii, wapo wanafunzi wengine wa kidato cha sita wamekosa mikopo, wapo wanafunzi wengine walio na diploma wamekosa mikopo" Amesema Rais Magufuli.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli pia amewataka wanafunzi wa vyuo mbalimbali hapa nchini kuacha kujihusisha na masuala ya siasa na badala yake wazingatie jukumu kuu lililowapeleka vyuoni ambalo ni kusoma, huku akibainisha kuwa serikali yake haitavumilia vitendo vya vurugu vyuoni.

"Ifike mahali watanzania tukubali ukweli, tuache siasa kwenye masuala ya msingi, ukimpeleka mwanafunzi wa kidato cha nne mwenye ufaulu wa divisheni 4, anachukua digrii, akishatoka pale, hata kama atafanikiwa kupata digrii itakuwa ni ajabu.


"Lakini niwaombe wanafunzi mahali kote, msitumiwe na wanasiasa, mmekuja kusoma, someni, siasa mtazikuta mkiondoka, nawambia mmekuja kusoma someni, na ndio maana hata katika kutoa mikopo hatubagui, sijui huyu CCM, sijui huyu CHADEMA, sijui huyu nini, nyie wote ni watanzania, ndio lengo letu. Amesisitiza Dkt. Magufuli.

Amewaahidi kuwa serikali yake itahakikisha inatoa mahitaji ya wanafunzi ikiwemo mikopo na kuboresha miundombinu ya vyuo, lakini amewataka wanavyuo nao kuwa wavumilivu na wazalendo pale ambapo mahitaji hayo yatachelewa kutokana na mchakato wa kuyapata kuhitaji muda.

Kabla ya kuwahutubia wanajumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Mkuu wa chuo hicho ambaye ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemuomba Rais Magufuli asaidie kuboresha miundombinu ya chuo hicho ikiwemo ujenzi wa mabweni ya wanafunzi ambao kwa takribani asilimia 70 wanaishi nje ya chuo, ambapo Rais Magufuli ameahidi kutoa shilingi bilioni 10 na ameuagiza uongozi wa chuo hicho kuainisha eneo ndani ya chuo ili ujenzi wa mabweni uanze mara moja.

Uzinduzi wa ujenzi wa Maktaba hiyo ya kisasa umehudhuriwa na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing ambaye nchi yake ndio imetoa msaada wa dola za Marekani zaidi ya Milioni 41 kwa ajili ya ujenzi wa Maktaba hiyo.

Maktaba hiyo ya kisasa itakapokamilika itakuwa ndio maktaba bora kuliko zote barani Afrika, ikiwa na ukubwa wa eneo la meta za mraba 20,000 na itakuwa na uwezo wa kuwa na vitabu 800,000 na kuchukua wanafunzi 2,600 kwa mpigo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Chuo hicho Profesa Rwekaza Mukandala, Balozi wa China hapa nchini lu you Qing, maafisa wa kampuni ya Kutoka China ya Jiangsu Jiangdu wakiweka mchanga kama ishara ya kuweka jiwe la msingi katika Maktaba Mpya ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UD) mara baada ya kuwasili chuoni hapo. Maktaba hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 2000 kwa wakati mmoja.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wa Chuo hicho Profesa Rwekaza Mukandala, Balozi wa China hapa nchini lu you Qing, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na makamu wa Rais katika serikali ya awamu ya nne Mohamed Gharib Bilal, Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Spika Mstaafu Pius Msekwa mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Maktaba hiyo ya kisasa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini katika Kitabu maalum cha Kampuni ya Jiangsu Jiangdu construction group inayojenga Maktaba Mpya ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam UD mara baada ya kuwasili chuoni hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Balozi wa China hapa nchini lu youQing kabla ya kwenda kuzungumza na jamii ya wanachuo kikuu cha Dar es Salaam.


Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala akitoa maelezo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa Maktaba hiyo ya kisasa itakayochukua wanafunzi zaidi ya 2000 kwa wakati mmoja. Wengine katika picha ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Wziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye mabango ya picha za mfano wa majengo ya Maktaba mpya itakayojengwa katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya jamii ya wanachuo na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Maktaba mpya itakayochukua zaidi ya wanafunzi 2000 kwa wakati mmoja.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli machapisho ya tafiti mbalimbali za madini na mambo mbalimbali ya kimaendeleo zilizofanywa na wahadhiri wa chuo hicho mara baada ya kuwahutubia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha machapisho hayo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya Wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya kumaliza kuwahutubia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba mara baada ya kumaliza mkutano huo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Mlimani jijini Dar es Salaam.

Rais Dk. John Magufuli (katikati), akiweka udongo kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa maktaba ya kisasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dar es Salaam leo asubuhi. Wengine wanaoweka udongo huo kutoka kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mkandara, Mkuu wa chuo hicho, Dk. Jakaya Kikwete, Balozi wa China nchini Tanzania, Mr.Lu na Meneja wa Ujenzi wa makataba hiyo.

Mkuu wa chuo Kikuu cha UDSM, Rais mstaafu Dk.Jakaya Kikwete akiweka saini wakati akiwasili kwenye hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi wa makataba hiyo.

Mkuu wa chuo hicho, Dk.Jakaya Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako (kushoto) na Makamu wa Rais mstaafu Dk. Mohamed Gharib Bilal.

Rais Dk.John Magufuli (katikati), akiwa na viongozi wengine wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi.

Rais Dk.John Magufuli (katikati) akiwa katika picha na viongozi mbalimbalimbali pamoja na wakandarasi wa mradi huo.

Rais Dk.Magufuli (katikati), akisalimiana na Makamu Mkuu wa Chuo cha UDSM, Profesa Mkandala (kulia). Kushoto ni Mkuu wa chuo hicho, Dk. Jakaya Kikwete.

Rais Dk.Magufuli akisalimiana na wakandarasi wazalendo.
Rais Dk.Magufuli, akiteta jambo na Balozi wa China Mr Lu.

Rais Dk.John Magufuli akisalimiana na wageni mbalimbali.

Wimbo wa taifa ukiimbwa.

Wadau na maprofesa mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.

Wakandarasi wa kichina wanao jenga maktaba hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.

Viongozi wastaafu wa chuo hicho wakiwa kwenye hafla hiyo.

Maprofesa mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la makataba hiyo.
 
Toggle Footer
TOP