Pia amewaagiza watendaji wote wa Serikali, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari, Maofisa Elimu, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa, kuhakikisha michango hiyo inayotolewa inawafikia walengwa.
Aidha, amezitaka wilaya zote nchini zianzishe mpango endelevu wa kuhakikisha kwamba upungufu wa madawati unasahaulika kabisa katika maeneo yao na kwamba utendaji wa viongozi wa elimu na Serikali katika ngazi mbalimbali utapimwa kutokana na jinsi ambavyo wametekeleza maagizo hayo.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumamosi, Juni 11, 2016) wakati wa matembezi ya hisani ya kukusanya fedha za kununulia madawati kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Katika maadhimisho hayo yaliyoanzia BOT hadi viwanjja vya Mnazi Mmoja, Gavana wa BOT, Profesa Benno Ndulu alimkabidhi Waziri Mkuu hundi ya shilingi milioni 263 zilizochangwa na benki hiyo pamoja na watumishi wake kama mchango wao kwa ajili ya ununuzi wa madawati.
Waziri Mkuu aliwapongeza watumishi wa BOT kwa kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto hiyo ambapo alitoa wito kwa taasisi zote katika sekta ya umma na binafsi pamoja na watu binafsi kuchangia uboreshaji wa elimu nchini kama sehemu ya “Majukumu ya Taasisi kwa Jamii” (Corporate Social Responsibility).
Amesema kuwa na elimu bora, siyo tu faida kwa Taifa, bali kwa waajiri pia, kwani itahakikisha kwamba taasisi za umma na binafsi zinapata wafanyakazi ambao wameiva na wenye weledi wa kutekeleza majukumu mbalimbali ya uzalishaji katika taasisi hizo.
“Nitoe wito pia kwa wanafunzi wote ambao watafaidika na kuboreshwa kwa mazingira ya kusomea, ikiwemo kupewa madawati na mahitaji mengine, kuhakikisha wanasoma kwa bidii kwa faida yao na Taifa kwa ujumla na kwa kufanya hivyo, wanafunzi watakuwa wanaenzi jitihada za Serikali, taasisi za umma, taasisi binafsi na watu binafsi katika kuboresha elimu nchini,” amesema.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeazimia kupambana na changamoto za sekta ya elimu na kwamba tangu Uhuru, Serikali za Awamu zote zimekuwa zikifanya jitihada mbalimbali katika kuboresha elimu kwa wananchi wake.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na wasanii wa Benki Kuu baada ya kuongoza matembezi kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu hadi viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016. Zaidi ya shilingi milioni263 zilichangwa.
Bendi ya Poli ikiongoza matembezi ya kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu hadi viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016.Zaidi ya shilingi263 milioni zilichangwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza matembezi ya kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu ha viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016.Kushoto kwake ni Gavana wa Benki Kuu, Benno Ndulu na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. Zaidi ya shilingi milioni 262 zilichangwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuongoza matembezi ya kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu hadi viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016. Zaidi ya shilingi milioni 263 zilichangwa.
- Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu