Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere, Butiama, Mara


KUANZA kwa Chuo Kikuu cha Kilimo na Sayansi cha Mwalimu Julius K.Nyerere kilichopo wilayani Butiama mkoa wa Mara kitaupandisha na kuuinua mkoa katika masuala mbalimbali pamoja na kuwasaidia wakulima katika kuinua kilimo.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Mara, Magesa Mulongo alipotembelea sehemu ya majengo ya iliyokuwa shule ya Osward Mang'ombe High School ambayo yatatumika kama "campas"ya chuo hicho kinachotarajiwa kuanza kupokea wanafunzi oktoba mwaka.

Amesema chuo hicho ambacho kitatoa shahada na stashahada za fani mbalimbali licha ya masuala ya kilimo itakuwa chachu kubwa ya maendeleo ya mkoa wa Mara na wananchi watakaokuwa wanazunguka mazingira ya chuo na kuwataka wananchi kujiandaa kukipokea.

Mulongo ambaye alikuwa ameongozana na viongozi wa ngazi ya wilaya,alisema cha kwanza ambacho kinapaswa kuangaliwa ni kuhakikisha migogoro ya aina yoyote baina ya chuo na wananchi haipatikani yakiwemo masuala ya ardhi ili uongozi wa chuo ufanye shughuli zake bila kubugudhiwa.

"Kwanza ni heshima kubwa kuwepo na kuletwa kwa chuo hiki mkoa wa Mara na hususani kwenye wilaya ya Butiama katika kumuenzi mzee wetu Mwalimu Julius Nyerere na ni muhimu kinapokwenda kuanza kusiwepo na vikwazo vya aina yoyote.

"Lakini chuo hiki kitaupandisha na kuuinua mkoa wa Mara maana mahala popote palipo na vyuo au chuo kikuu licha ya mkoa kunufika lakini pia wananchi wananufaika kutokana na fursa mbalimbali ambazo watazipata kutoka kwa wanachuo,"amesema Mulongo.

Amesema kutokana na taarifa ambazo amepewa na uongozi wa chuo hicho,wananchi wakulima wa kawaida pia watapata fursa ya kupata kozi fupi ambazo zitawasaidia kuboresha shughuli zao za kilimo na kuwaomba wananchi kujiandaa na hilo.

Akitoa taarifa ya chuo hicho baada ya kuteuliwa na Rais wa awamu ya nne,Jakaya Mrisho Kikwete,kuanza mchakatato wa chuo hicho,Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaruma,profesa Lesakit Mellau,amesema wameshafikia hatua kubwa ya kuanza kwa chuo hicho ikiwemo kuanza kuajili wahadhiri.

Amesema bado kuna masuala ya fedha kutoka serikalini yasubiliwa kutokananza kupokea na bajeti na mambo yakienda vizuri kufikia oktoba wataanza kupokea wanafunzi.

Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Butiama waliozungumza na Mtanzania kuhusiana na chuo hicho walisema wapo tayari kutoa ushirikiano kutokana na manufaa ambayo watayapata kutokana na kuwepo kwa chuo hicho katika maeneo yao.


Mulongo alipokuwa akiingia maeneo ya chuo hicho

Sehemu ya majengo ya chuo


  • Imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Shommi B.