He! Ushirikina tena kwenye nyimbo za Injili?


MWIMBAJI wa nyimbo za Injili, Madam Ruth Mwamfupe ‘Madam Ruth’, ameweka wazi kwamba wasanii wengi wa muziki huo ni wafitini kutokana na kujihusisha katika masuala ya kishirikina na kuitenga imani yao.

Akizungumza na MTANZANIA, Madam Ruth anayetamba na wimbo wake wa ‘Jana Imepita’, alisema alidhani mambo hayo hufanywa na wasanii wa muziki mwingine lakini ajabu yanafanyika katika muziki wa Injili.
“Kumekua na ufitini mwingi kwenye huduma hii ya uimbaji, inadaiwa wapo wanaokwenda kwa waganga wa jadi kwa ajili ya kuzima nyota za waimbaji wengine jambo ambalo ni kinyume na mpango wa Mungu na wanaofanya hivyo wanapaswa kuacha kwani mwisho wao si mzuri,” alisema msanii huyo.