Loading...
Sunday

Idrisa Kweweta aeleza sababu ya umaskini wetu Watanzania

Hatuwezi tukapiga hatua endelevu kama tunaamini umaskini wetu utaisha kwa kuwa pesa nyingi, hata kama tukiwa na fedha kila kona ya nyumba zetu bado umaskini ufakuwa unabisha hodi.

Japokuwa kina Karl Marx wanasema, "Njaa au umaskini ni zao la kutokuwa na mgawanyo sawa wa mali na ulimbikizaji wa mali kwa watu wachache (mabepari)," umaskini hutokana na uongozi na usimamizi mbovu ambao unawanyima umma fursa ya kutumia raslimali.

Nakubaliana nao katika usimamizi, lakini bado ninaamini umaskini ni zao la ukosefu wa maarifa, stadi na fikra ama mtazamo sahihi katika kupambanua changamoto, matatizo na majaribu kuwa potential.

Umaskini wetu Watanzania siyo kwa sababu hatuna mali au hatumiliki kitu (possession) ni kwa sababu hajui kitu, kwa maana pana tumekosa maarifa, stadi (njia bora za uzalishaji na usimamizi wa mali) na kutawaliwa na fikra au mitazamo ya kushindwa (deficit mindsets).

Mstari huu ndio unaotumika ktk utabakishaji wa nchi ulimwengu wa kwamba nani anajua ni nini na siyo nani anamiliki nini.

Narudia tena, umaskini wetu hatutoutibu kwa fedha, bali lazima tubadili fikra zetu ambazo zinatufanya tuamini pesa ndiyo kila kitu.

Ijumaa karimu
 
Toggle Footer
TOP