Jibu la swali kuhusu "...utaratibu kwa kujiunga na Jeshi la Polisi ...nimehitimu JKT"

Juzi mdau O.H.M. (majina kamili yamehifadhiwa) alituma ujumbe ufuatao:
Mim ni mwanafunzi ambae nilikuwa nikisomea diploma maalum ya elimu ya sekondary sayansi, hisabati na tehama ila kulingana na sababu mbalimbali imetokea kufunga kwa chuo hicho kikuu cha Dodoma hivyo nilitaka kufahamu utaratibu kwa kujiunga na jeshi la polisi kwani nimehitimu jkt *** *** katika operasion ya miaka 50 ya jkt na kupata namba **:**** cheo SM jina kamili O.H.M.
Regards,
O.H.M (email imehifadhiwa)
Nimeulizia kunakohusika na kupata maelezo yafuatayo:
Maelezo ni kwamba asubiri hadi hapo Jeshi litakapotangaza Ajira za jeshi la Polisi ambapo sifa zitaainishwa ikiwa ni pamoja na wale waliopitia JKT.