Loading...
Wednesday

Jihadhari! Operesheni kukamata wanaoendeshea service rd na BRT

UPDATE, Juni 2, 2016:
Kuna huyu ameandika hivi leo,
"Jamani kama mna tabia ya kutanua au kuchepuka brbrni acheni kabisa...... Yaliyonikuta leo sitasahau... Tangu 12 kasoro tuko polisi hadi jioni hii ndio wanatutoa na fain juu.. Tena tumepona kwa rehma za Mola mana wenzetu wengine wanapelekwa mahakamani kesho....Ofsini pia hatukwenda leo na mwenzangu...."
Kuna operesheni Jiji zima la Dar kwa wanaotanua/wanaopita/wanaochepuka na service road na njia ya mabasi yaendayo haraka.

Kuweni makini.

RTO wa Kinondoni anakamata yeye mwenyewe. Ukidakwa unalala "locked-up" na kesho yake unapelekwa mahakamani. Ujue ukikamatwa HAKUNA DHAMANA Polisi.

Just for your info.

UJUMBE HUO UMEHAKIKISHWA:
Ni kweli kabisa @Subby Operation hiyo ipo na anasimamia Yeye mwenyewe na kuhakikisha anayefanya kosa anapelekwa mahakamani na siyo kulipa fine. Na sasa hivi sio RTO Kinondoni tena bali ni ZTO (Zone Traffic Officer). Ana mamlaka jiji lote (Ilala, Temeke, Kinondoni). Tujitahidini tu kufuata sheria.
----
via WhatsApp
 
Toggle Footer
TOP